Meneja uhusiano
wa Airtel Tanzania Jackson Mbando
akiongea na waandishi wa Habari wakati wa kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya
mpira wa soka ya Manchester United ambayo itafanyika Jijini Dar es Salaam April
23-27 chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United. Kushoto ni Rais wa
shirikisho la mpira wamiguu nchini (TFF) Jamal Malinzi. Iliofamyika jijini
Dar-es-Salaam leo.
Rais
wa shirikisho la mpira wamiguu nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongeana na waandishi wa habari wakati wa
kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya mpira wa soka ya Manchester United ambayo itafanyika Jijini Dar
es Salaam April 23-27 chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United.
Kulia ni meneja uhusino wa Airtel Tanzania Jackson Mbando.
===***===
·
Ni
kutoka nchi 12 Afrika
·
Waziri
Bernard Membe mgeni rasmi siku ya ufunguzi
·
Kliniki
kuendeshwa na makocha kutoka Manchester United
Wachezaji wa soka chini ya umri wa miaka 17
kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam
Jumatatu Aprili 21 kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa. Hii ni mara ya pili Tanzania imepewa heshima
ya kuwa mwenyeji wa kliniki ya kimataifa baada ya ile iliyofanyika kwenye
uwanja wa wa kisasa wa Taifa mwaka 2011.
Kliniki
ya mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam inakutanisha wachezaji chipukizi, wasichana na wavulana,
kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville,
DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania.
Mafunzo
hayo ya siku tano mfululizo chini ya makocha wazoefu kutoka klabu maarufu
duniani ya Manchester United yana lengo la kuwapa vijana mbinu mbalimbali za
kisoka hasa katika eneo la ushambuliaji.