Mtu mmoja amefariki dunia na 19 wamejeruhiwa na kuporwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na fedha baada ya majambazi kufunga barabara kwa mawe na magogo na kisha kuteka magari katika eneo la mkata doma barabara ya morogoro iringa.
Nae mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro Dr Erick Rwegoshora amekiri kuwepo kwa taarifa za kifo na wamepokea majeruhi wengine wamelazwa na wengine walitibiwa na kuruhusiwa .