Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha Hassan Silayo)
====*****====
|
Na Frank Mvungi
Serikali imekanusha taarifa za upotoshaji kuwa imesititisha matumizi ya mashine za Kielektroniki ( EFD's) hapa nchini.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Mjanga wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza
Bw. Julius amesema taarifa kuwa matumizi ya mashine za kielektroniki
yamesitishwa ni upotoshaji na hayana ukweli wowote.
Akifafanua
zaidi Bw. Julius amesema kwa kuthibitisha kuwa taarifa hizo si za kweli
kwani mnamo tarehe 26Februari 2014,Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
aliitisha kikao kati ya TRA,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda na
biashara pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) .
Bw.
Julius alibainisha kuwa katika kikao hicho Mh. Waziri Mkuu alielekeza
kuwa orodha ya wafanyabiashara walioainishwa na kupewa barua iwekwe wazi
kwa kubandikwa katika ofisi zote za TRA za Mikoa na Wilaya.
Pia
Bw. Julius alisema kufuatia maelekezo hayo Mamlaka yaMapato Tanzania
imeendelea kusimamia utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya EFds
unaoendelea na orodha ya wafanyabiashara husika ipo katika mbao za
matangazo ya ofisi za TRA za Mikoa na Wilaya zote pamoja na kwenye
tovuti.
Aliongeza
kuwa TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini wenye sifa za
kutumia mashine za kielektroniki ambao ni wa lengwa katika awamu ya pili
kuzitumia kama sheria inavyotaka.
Bw.
Julius aliwataka wananchi kutoa taarifa katika mamlka hiyo pale ambapo
watatakiwa kutoa rushwa au kubugudhiwa wanapohitaji huduma katika ofisi
za mamlaka hiyo kutoa taarifa katika vyombo vya dola au katika ofisi za
TRA kupitia simu namba 0689122515 au ujumbe mfupi kwenye namba
0689122516.