SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 3, 2014

MATUKIO MBALIMBALI YA KAMPENI ZA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE KUPITIA CHADEMA

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Issa Said Mohamed akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Miono, katika mkutano wa kampeni, uliofanyika kijijini hapo jana.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Miono wakiitikia kauli mbiu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ya "Peoples Power" wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Miono jana

 Mgombea ubunge wa Chalize kupitia CHADEMA ndugu Mathayo Torongey akisalimiana na wakazi wa Lugoba Jimboni Chalinze.
 Kiongozi wa kimila wa wamasai, Tikwa Moreto (aliyeketi), akishiriki kumwombea mgombea wa ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Dempkrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey (wa tatu kushoto), nyumabni kwa kiongozi huyo kijiji cha Gumba, Kibaha Vijijini leo.
Kiongozi Mkuu wa kimila wa wamasai, Tikwa Moreto (kushoto), akiongozana na mgombea wa ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Issa Saidi Mohamed walipokwenda nyumabni kwake kwa jaili ya kuomba baraka zake leo.Picha Zote na Chadema