Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma akipokewa na ujumbe
wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa siku mbili baina ya Afrika na Ulaya
mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Sheraton huko Brussels nchini
Ubelgiji akitokea nchini Uingereza tarehe 2.4.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenza wa
mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Ubelgiji.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Madagascar Mama
Lalao Rajaonarimampianina muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye chakula
cha mchana kilichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa Afrika kwa ajili ya
wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa
Afrika na Ulaya unaofanyika huko Brussels tarehe 2-3.4.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadaye wakibadiishana mawazo
na Mke wa Rais wa Congo Mama Antoinnethe Sassou Nguesso wakati wa hafla
ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Jumuia ya wenza wa mabalozi wa
Afrika wanaowakilisha nchi zao huko Ubelgiji tarehe 2.4.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Cameroon Mama
Chantal Biya muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye chakula cha mchana
walichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha
nchi zao huko Ubelgiji kwenye hoteli ya Sheraton tarehe 2.4.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipokea cheti maalum cha ulezi wa heshima wa
Chama cha wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika walioko nchini Ubelgiji
(Honory Patronese of the Association of the Spouses of African
Ambassadors in Belgium) kutoka kwa Mke wa Balozi wa Cameroon nchini
Ubelgiji Mama Christiane Eloundov de Evina wakati wa chakula cha mchana
walichowaandalia wake wa Marais wa Afrika jijini Brussels tarehe
2.4.2014.
Mke wa
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mama Adelaida Kamala akimkabidhi
Cheti Maalum cha ulezi wa heshima cha wenza wa mabalozi wa Afrika
walioko Ubelgiji, Mke wa Rais wa Cameroon Mama Chantal Biya wakati wa
chakula cha mchana walichowaandalia wageni hao kwenye hoteli ya Sheraton
tarehe 2.4.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa Marais
na Wakuu wa nchi za Afrika pamoja wa wenza wa Mabalozi wa nchi hizo mara
baada ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenza hao tarehe
2.4.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.