Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro (kushoto) akiwahutubia wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (wa pili kushoto) akitoa hotuba yake kwa wanamahafali wa mafunzo ya jinsia katika chuo cha GTI leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro pamoja na Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) wakiongoza maandamano ya wanamahafali ya pili ya Chuo cha GTI kuelekea ukumbuni kabla ya kuanza kwa hafla hiyo
Mkuu wa taaluma na mipango wa GTI, Bi Doroth akitamka kuanza kwa sherehe za Mahafali ya Pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia Tanzania (GTI) kwenye hafla ya mahafali hayo leo.Sehemu ya wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) wakiwa kwenye sherehe za mahafali yao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Mabibo jijini Dar .
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro (kushoto) akimtunuku cheti cha jinsia mmoja wa wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam
Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya kutunukiwa
Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akikabidhiwa cheti chake mara baada ya kutunukiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro .
Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya kutunukiwa.Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) akinong'ona jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro kwenye sherehe za mahafali ya pili ya Chuo cha GTI leoMwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro, Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wanamahafali baada ya kutunukiwa vyeti vyao.Wanamahafali wakiimba wimbo wa taifa kabla
ya kuanza kwa sherehe za mahafali yao leo.
Na Thehabari.com, Dar es Salaam MAHAFALI ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) yamefanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho eneo la Mabibo. Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 9 wamehitimu mafunzo ya njinsia ngazi ya cheti. Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro alikipongeza chuo hicho kwa kuendelea kutoa mafunzo ya jinsia nchini kwa ngazi mbalimbali jambo ambalo linawezesha wahitimu kuwa na uwezo wa kuchambua na kutathmini sera na program anuai kwa mtazamo wa kijinsia katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Aliutaka uongozi wa GTI kwa kushirikiana na bodi kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo hicho, ikiwemo changamoto za uhaba wa raslimali watu na fedha ili kuhakikisha malengo ya chuo hicho ya kudahili wanafunzi wengi zaidi yanafikiwa na kuanza kwa wakati.
"..Rai yangu niwaombe wewe mkuu wa chuo kwa kushirikiana na bodi ya GTI mfanye kila liwezekanalo ili kuwezesha mafunzo hayo kuanza mapema na hatimaye wanafunzi hawa na wengine watakaopenda kuendelea na masomo yao hapa chuoni wafanye hivyo ili kutimiza ndoto zao na matarajio yao," alisema Bi. Muro.
Aidha aliwapongeza wahitimu kwa kufanikiwa kumaliza mafunzo yao na kuwataka wakaitumie elimu hiyo kiufasaha kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kuwa wataalamu na mabalozi wazuri wa masuala ya jinsia hapa nchini.
"...Nitumie fursa hii kuwaomba mkawe wataalamu na mabalozi wazuri wa masuala ya jinsia hapa nchini na kwa kufanya hivyo nchi itajivunia utaalamu wenu ambao kama utatumika vizuri utaiwezesha jamii kuwa na mipango na utekelezaji wa shughuli za maendeleo...," alisisitiza.
Naye Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo akizungumza na wahitimu na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha utekelezaji wa mipango yake kikamilifu, hivyo kuiomba Bodi ya chuo kusaidia kutatua changamoto hizo ili chuo kiendelee kufanya vizuri zaidi katika mipango yake. Mahafali hayo ya Chuo cha GTI ambacho kinaendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) pia yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao, Mary Rusimbi, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi, wafanyakazi wa GTI na TGNP Mtandao pamoja na wageni waalikwa
NA ANKAL MICHUZI