SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 22, 2014

MAENDELEO YA MSIBA WA MHE. MOSHI MUSSA CHANG'A, NYUMBANI KWA MAREHEMU MBAGALA JIJINI DAR JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya akiwa ni mwenye majonzi wakati akisaini kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari.  

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu,eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo taratibu zote zinafanyika hapo.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba Shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu,Mhe. Moshi Mussa Chang'a itafanyika leo Aprili 22,2014 nyumbani kwake Mbagala na baadae mwili utasafirishwa kwenda kijijini kwao Mkoani Iringa kwa Mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwassa wakati wakiwa kwenye Msiba wa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a,nyumbani kwa Marehemu Mbagala,jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya Waheshimiwa wakuu wa Wilaya mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye msiba wa Mkuu mwenzao wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia juzijioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari,nyumbani kwa Marehemu Mbagala jijini Dar es salaam.

========
TANZIA: MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MHE. MOSHI MUSSA CHANG'A AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO (Sunday, April 20, 2014 )
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo enzi za uhai wake Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari. 

Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)