SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 3, 2014

Ankal avamia BBC London

 Ankal akiwa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Bw. Ali Saleh alipovamia kituo hicho kuwataka hali wadau. Ankal alifarijika na kufurahi mno kukuta kumbe bosi huyu ni Bwawa la Maini damu kama yeye. Ila alimkuta hana furaha sana  kwa kuwa vijana wa Liverpool wameharibu plani ya kocha Brendan ya kubaki katika nne bora tu mwaka huu ili kucheza Europe Cup na sio kuchukua ubingwa mwaka huu. Maana inavyoelekea kombe linaenda Anfield, ambapo Ali Saleh anasema ah! tukishinda hatutolikataa ila sie tumepanga tulibebe mwakani na sio mwaka huu....!
 Charles Hilary Mkwanda akicheza na Ze Fulanazzzzzzz
 Ankal na Bi Zuhura Yunus. Kumbe bado katoto kadogoooo.....dah!
Ankal na  Salim Kikeke a.k.a 'Yul Bryner.
 Ankal akila selfie na wadau Mariam Omar na Peter Musembi.
 Ankal akiwa na Alex Muriethi (aliyeketi) na 'shemeji' yetu Siraj Kalyango ambaye chupuchupu amuoe nanihii, ila alichelewa kuleta mahari, na mke kusombwa na maji mengine...
Ankal akila konozzzzz na Zawadi Machibya. Anatoa shukurani sana kwa BBC idhaa ya Kiswahili kwa ukarimu na ucheshi wao na kumpokea kwa moyo mkunjufu japo alifika hapo bila taarifa wala mihadi. Pia hapo BBC idhaa ya Kiswahili wana utamaduni wa kumkaribisha mdau yeyote kutoka Afrika kwa moyo mkunjufu na hata kumfanyia mahojiano kama inawezekana.