
Raia wa China wanaotuhumiwa kukutwa na pembe za ndovu zaidi ya vipande
700 wakisubiri kuanza kwa shauri lao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory
---
Raia wa China, Huang Gin, Xu Fujie na Chen Jinzha wamedaiwa
kutoa hongo ya Sh30.2 milioni kwa polisi na askari wa wanyama pori ili
wasipekue nyumba waliyokuwa wakiishi iliyo Mtaa wa Kifaru Mikocheni.
Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na nyara za
Serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa
kilogramu 1,880 vyote vikiwa na thamani ya Sh5.4 bilioni.
Shahidi wa upande wa mashtaka, ambaye jina lake
limehifadhiwa kutokana na amri ya Hakimu Isaya Arufani wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Kisutu iliyotolewa jana ya kuvitaka vyombo ya habari
kutotaja majina ya mashahidi watakaotoa ushahidi kwenye kesi hiyo,
alidai kushuhudia tukio hilo.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.....
0 comments:
Post a Comment