SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, March 4, 2014

LICHA ZA MOJA KWA MOJA KUTOKA KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA LEO: MWENYEKITI WA CHADEMA AITABIRIA CCM USHINDI WA KISHINDO



 Mgombea ubunge Jimbo la Kalemnga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (kushoto) akijiunga kucheza ngoma ya asili ya kabila la wahehe iliyokuwa ikiongozwa na msanii maarufu wa filamu na muziki, Dokii wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kalenga leo katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini .Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema wa Kijiji hicho aliitabiria CCM ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
 Ofisa wa CCM Makao Makuu ya Umoja wa Vijana, Mwampamba ambaye alijitoa Chadema, akielezea kisa cha kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga na CCM.
 Mwenyekiti wa Chadema katika Kijiji cha Lupembelwasenga, Ezekiel Kibiki 9kushoto), akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo na kuamua kujiunga na CCM leo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Kalenga. Kibiki aliitabiria CCM ushindi katika uchaguzi huo. Pia amesema kuwa tayari amewashawishi wanachama wengine wa Chademe kujiunga na CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo, akichuchumaa ikiwa ni heshima ya kumuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akielezea mikakati ya chama hicho  kukigalagaza chama Chadema katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga leo mchana katika Kijiji cha Kikombwe, Iringa Vijijini.
Godfrey Mgimwa akijinadi katika mkutano wa  kampeni leo katika Kijiji cha Kikombwe.

Wananchi katika Kijiji cha Kikombwe wakimsikiliza Mgimwa kwa makini
 Wananchi wa Kijiji cha Kikombwe wakinyoosha mikono kuthibitisha kumchagua mgombea wa CCM katika jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano uliofanyika katika kijiji hicho.

 Msanii Dokii (kulia)akihamasisha wananchi katika kijiji cha  Lupembelwasenga
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Salum Mtenga akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo, kuhusu mambo yanavyoendelea katika kampemni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga. Picha zote na Richard Mwaikenda na Bashir Nkromo
--
NA BASHIR NKOROMO, KALENGA
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Lupembelwasenga, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Kibiki, ameitabiria CCM kumiminiwa kura za kishindo na wananchi wa kitongoji hicho katika uchaguzi mdogo wa
ubunge utakaofanyika jimboni humo Machi 16, mwaka huu.

Amesema, uhakika huo anao kutokana na yeye na wananchi wengi wa kitongoji hicho kubaini kwamba CCM ikiahidi jambo inatekeleza na ndiyo yenye ilani inayotekelezwa kwa sasa tangu ilipopewa ridhaa na wananchi ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu uliopita, tofauti na Chadema ambao alidai ahadi zao ni za uongo na hawana kazi ya kufanya katika shughuli za maendeleo.

Mwenyekiti huyo wa kitongoji kwa tiketi ya Chadema, alisema, hayo leo, Machi 4, 2014, kabla ya kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM, katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye kitongoji hicho, kumnadi mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa.

"Hivi sasa natangaza kuhama Chadema, na nina kuhakikishieni kwamba wapo watu wengi nyuma yangu ambao tumeachana na chama hicho na sote kwa jumla tumeahidi wananchi wa kitongoji chetu kuifanya CCM iibuke na ushindi wa kishindo kwa kuimwagia kura zetu nyingi katika uchaguzi huu, anayefikiri natania asubiri ataona baada ya uchaguzi", alisema Kibiki.
Kibiki alisema, yeye na wenzake wameamua kuachana na Chadema baada ya kubaini kwamba, maneno ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi wa chama hicho ni ulaghai mtupu ambao ukifuatwa unawapotezea muda wananchi katika kujiletea maendeleo.

Alisema, baada ya kutafakari kila mmoja kwa wakati wake, wamebaini kwamba, CCM ndicho chama chenye uhakika wa kusimamia maendeleo yao, kwa sababu kiliwaahidi kujengwa barabara nzuri na sasa ipo, mbali na mambo mengine ambayo yametekelezwa kupitia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Kalenga na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa ambaye alifariki dunia Januari Mosi, mwaka huu.

Baada ya kutangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM, Kibiki alikabidhi kadi yake, kwa Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Delfina Mtavilalo, hatua iliyofuatiwa na wanachama wengine tisa wa Chadema kutoka kitongoji hicho nao kukabidhi kadi zao kwa Mwenyekiti huyo.

Akizungumza na wananchi kwenye mkutano huo, Mgombea wa CCM katika uchaguzi huo wa Kalenga, Godfrey Mgimwa alisema, anatambua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, ndiyo sababu amejitolea kuipeperusha bendera ya CCM ili akipata fursa ya kuchaguliwa asimamie kuzitatua.

Mgimwa alisema, miongoni mwa changamoto ni uendelezaji wa ujenzi wa zahanati na shule katika Kitongoji hicho, ambao ulikuwa umeanzishwa na Mbunge wa zamani Dk. Mgimwa.

Alisema, ana uhakika kwa kupata ushirikiano wa wananchi na mwongozo wa ilani ya CCM ya mwaka 2010, ana uhakika changamoto hizo na nyingine zilizopo atapambana nazo hadi kuhakikisha zinapungua au kwisha kabisa.

0 comments:

Post a Comment