SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, March 4, 2014

AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI

 Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake.
 Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani).
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando
 Akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya  mitambo mipya inaotumiwa na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa maji safi na salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
 Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi.
 
 ====****====
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,Jakaya Kikwete Akagua madaraja ya kijeshi yakiwemo yale ya kuelea juu ya maji wakati alipokagua zana za kijeshi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua madaraja ya kijeshi yakiwemo yale ya kuelea juu ya maji wakati alipokagua zana za kijeshi jana, Jumatatu, Machi 2, mwaka huu, 2014.Picha na Freddy Maro-IKULU
 

0 comments:

Post a Comment