SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, March 1, 2014

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR: JE HAWA NI SAHIHI KUWEPO KATIKA ENEO HILI?‏

Hili ni eneo la Kituo cha Daladala cha  Ubungo jijini Dar, biashara ndogondogo zikiwemo za viatu zinafanyika wakati huo huo waenda kwa miguu nao wakipita eneo hilohiolo.
...Wengine wanauza samaki katika eneo ambalo kiafya si sahihi.
Nguo za ndani zikiuzwa katika eneo hilo. Jambo ambalo husababisha msongamano katika eneo hili na wakati mwingine kuleteleza ajali zisizo za lazima.
...Suluali zikiwa zimetundikwa  pembezoni mwa barabara.
Bila kujali vumbi katika eneo hili, wauzaji wameanika T-Shirt zao na kuendelea kuuza.
....Wengine nao wanauza Urembo pamoja na vifaa vya simu.
Hii kali sana hawa Jamaa wanauza DVD kwa Tsh 500 hadi 1,000 bei ya juu. Swali linakuja hapa kuna kazi za nje na ndani ya Tanzania, Je Haki miliki Mpo? na watu wa mapato hili mnalionaje?
...Wauza Redio nao wapo.
Huu ni uzibe wa barabara kuu, ambapo pembezoni mwake waenda kwa miguu hupita wakati huo biashara ya nguo ikiendelea kuchukua nafasi.
Katika eneo hili la Ubungo sio pembezoni mwa barabara pekee lakini hadi mabondeni biashara zinaendelea.
Hawa nao wapo wanauza Vioo vya kujitazamia pamoja na vifaa vya kuegeshea nguo.
Mikanda na Boksa navyo vinauzwa katika eneo hili.
Miwani ya wakubwa na watoto nayo ipo kwa bei chee.
Bukta nazo zinauzwa eneo hili.
Hii ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya Gesi hadi eneo la kituo cha magari ya kwenda Mwenge.

Hili ni eneo la Ubungo ambapo Kumekuwa na kero kubwa ya wafanyabishara wadogo wadogo kuweka biashara zao za kila aina pembezoni mwa njia za wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Licha ya usumbufu huo  na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato chao bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na kutekeleza jukumu lao la wizi.

Wakizungumza na mtandao huu, watumiaji wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa husika kwa kushindwa kuwatafutia eneo husika wafanyabiashara hao. Kutokana na uzembe huo mkubwa wakutowazuia, nao wameamua kuendelea kuleta kero.
Je Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili ya kufanya biashara hizi?
"Eneo hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu la kuingia jijini na mara watu wanapoingia wanakutana na kero hii ambayo mimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwatafutia eneo husika hii ni aibu" .
Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara.
PICHA NA DAR ES SALAAM YETU

0 comments:

Post a Comment