Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Hondogo,Kata ya Mandera wakati wa muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,leo Machi 29,2014.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe,Suleiman Jaffo akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mandera Kibaoni wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo Machi 29,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akishiriki kuruka sambamba na wakina Mama wa Kabila la Wamasai,wakati alipowasili kwenye Kitongoji cha Nameloki Chatanga,Kijiji cha Umasaini,Kata ya Mandera.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Magole,Kata ya Mandera wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo Machi 29,2014.
Wananchi wa Kijiji cha Hondogo katika Kata ya Mandera ndani ya Jimbo la Chalinze,wakinyoosha mikono juu kuashiria kumpigia kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati Mkutano wa Kampeni zake zilizofanyika Machi 29,2014.Picha na Othman Michuzi.