Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masulala mbalimbali ya uhusiano wa kimataifa ikiwamo hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika kusuluhisha Migogoro inayotokea ndani na nje ya mataifa mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuingia katika mgogoro na majirani zake, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifanya mahojiano na Mwandishi wa
shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Erick David Nampesya leo Jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya waandishi wa
Habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Bernard Membe uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Hassan Silayo
0 comments:
Post a Comment