Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM kwa mwanachama mpya
wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha Chadenje aliyehama kutoka Chama Cha
Wananchi,CUF wakati wa sherehe za uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka
37 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa huko Kiwalala, wilayani Lindi
Vijijini tarehe 1.2.2013.
Furaha ya kadi ya CCM
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete
akimpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo, CHADEMA, Mkoa wa Lindi Bwana Ali Omar Chitanda, ambaye
amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Mama Salma
baada ya kumpongeza alimtambulisha kwa wananchi akiwa pamoja na Bi. Asha
Chadenje wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka y37 ya CCM mkoani Lindi
tarehe 1.2.2014.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Lindi Ndugu Ali Mtopa akitoa hotuba
fupi ya kumkaribisha Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ili aweze kuzindua
rasmi sherehe za kutimiza miaka 37 ya CCM kwa Mkoa wa Lindi kwenye Kata
ya Kiwalala huko Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014.
IMG
5076, 5119, 5189 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya
wanachama wa CCM na wananchi wa Lindi Vijijini wakati akizindua rasmi
sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi katika mkoa wa
Lindi. Shughuli hiyo ilifanyika katika kata ya Kiwalala iliyoko Lindi
Vijijini. Sherehe hiyo ilienda sambamba na kumnadi mgombea wa udiwani
kupitia Chama Cha Mapinduzi katika kata hiyo Bwana Shineni Hamis Zahoro
katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 9.2.2014.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea
wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
Baadhi ya wananchi katika sherehe hizo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Mkoa wa Lindi Bwana Ali Omar Chitanda,
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea
wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
Mgombea
wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
Mama Kikwete akimwaga sera za CCM
Kicheko
Ngoma
ya Tambiko inayochezwa na wananchi wa kabila la wamakonde nayo ilikuwa
ni kivutio tosha wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka 37 ya Chama Cha
Mapinduzi zilizofanyika kimkoa kwenye kata ya Kiwalala, Lindi Vijijini

wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ,Mama Salma
Kikwete akiteta jambo na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi
Dr.Maua Daftari (katikati) huku Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Lindi
Vijijini akisikiliza wakati wa uzinduzi rasmi wa kumbukumbu ya kutimiza
miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi zilizofanyika katika Kata
ya Kiwalala iliyoko Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014.
--------------------------
Mama Kikwete awataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa kutunza ardhi yao na siyo kuiuza kwa wageni
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi kuitunza ardhi nzuri na ya rutuba waliyonayo na kutokubali
kuiuza kwa wageni bali waitumie katika kilimo kwa kufanya hivyo
watajipatia chakula cha kutosha na hivyo kuepukana na tabia ya kuomba
chakula.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa aliutoa wito huo
jana wakati wa kilele za sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) zilizofanyika katika kata ya Likunja wilayani humo.
Mjumbe
huyo wa NEC alisema wilaya hiyo imejaliwa kuwa na ardhi nzuri na rutuba
ambayo mazao mengi yanastawi kwa wingi kama wananchi hao watumia ardhi
hiyo kulima mazao ya vyakula kwa wingi wataepukana na tatizo la njaa.
“Ardhi
ni mali na ikitunzwa vizuri itawatunza hapo baadaye itumieni kulima
mazao ya chakula kama mahindi, mihogo na mtu aone aibu kwenda kuomba
chakula kwa jirani kwani hata watoto wenu wakila chakula kizuri na
kushiba wataweza kuwa na afya njema na kusoma vizuri wawapo shuleni”,
alisema Mama Kikwete.
Akizungumzia
kuhusu CCM kutimiza miaka 37 Mjumbe huyo wa NEC aliwataka wakazi wa
mkoa wa Lindi kutembea kifua mbele na kujivuna kwani Serikali ya chama
chao imefanya mambo mengi ya maana ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
barabara, shule, hospitali na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake
ukilinganisha na miaka ya nyuma.
“Leo
hii kuna baadhi ya watu wanapita na kusema kuwa Serikali haijafanya
jambo la maana kitu ambacho si kweli kwani ukilinganisha na miaka ya
nyuma hivi sasa watoto wetu wanaomaliza darasa la saba wanajiunga na
elimu ya Sekondari kwa wingi kwani shule zipo.
Hivi
sasa barabara ni nzuri na ni rahisi kwa mtu kusafiri kutoka eneo moja
hadi lingine tofauti na miaka ya nyuma pia huduma ya afya imeimarika.
Nawaomba msiwe wanyonge tembeeni kifua mbele na pale mpakapoulizwa
jibuni hoja kwani majibu mnayo”, alisema Mama Kikwete.
Mama
Kikwete pia aliwataka wananchi hao kutunza amani, upendo na
mshikamano uliopo ili waweze kufika mbali kimaendeleo kwani vitu hivyo
wakivipoteza ni sawa na kupoteza lulu waliyonayo.
Amani
ikitoweka hakuna jambo lolote litakalofanyika zaidi ya watu kukimbia
huku na kule kunusuru roho zao, nchi zisizo na amani watu hawawezi
kukusanyika kwa pamoja na kufanya mambo yao pamoja na demokrasia iliyopo
nawashauri mjitahidi kuchagua vitu ambavyo vina maslahi ya Taifa.
Alisema,
“Hao wanaowashawishi ninyi mfanye vurugu mbona kwao kuna aman?, ni
ukweli kuwa mikoa ya Kusini ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini sasa neema
imepatikana baada ya kuendelea mnataka kurudi nyuma jitahidini kuwa
wazalendo na kutengeneza mazingira ya kujali kwenu kwa kufanya shughuli
za maendeleo angalieni msiwe chanzo cha matatizo katika maeneo
mnayotoka”.
Kwa
upande wake Mlezi wa Chama hicho katika mkoa wa Lindi Dk. Maua Daftari
aliwapongeza wanachama hao kwa kuweza kutekeleza ilani yao ambayo
imeweza kuwasaidia kufika miaka 37 na kusema kuwa wasisikitike na maneno
ya kashfa yanayotolewa na wapinzani kwani ndiyo siasa ya vyama vingi
ilivyo nao kama vyama vingine wamepata mdomo wa kusemea.
“Serikali
iliamua kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ingawa katika kura
zilizopigwa na wananchi asilimia 80 walikataa na asilimi 20 ya wananchi
walikubali lakini ilifanyika hivi ili wananchi wengine waweze wafanye
kazi kwa pamoja na Serikali kupitia vyama vyao vya siasa na hii ndiyo
demokrasia ya kweli”, alisema Dk. Daftari.
Naye
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mzee Ali Mtopa aliwataka wapinzani waache
tabia ya kukichafua chama hicho bali wakubali kuwa Serikali imefanya
mambo mengi ya maendeleo na siyo kutukana viongozi waliopo madarakani
bali kila mtu amwage sera za chama chake na siyo kashfa.
Wakati
huohuo Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya
Ruangwa Saidi Nng’umbanga ambaye alialikwa katika sherehe hizo
aliipongeza CCM kwa kufikisha miaka 37 na kuwa chama cha Demokrasia kwa
kuvishirikisha vyama vingine vya siasa katika mambo mbalimbali.
Nng’umbanga
alisema mikusanyiko ya wana Lindi na Mtwara ni ishara kuwa katika mikoa
hiyo kuna amani ya kutosha na hakuna uhasama miongoni mwa watu kwani
wanakutana katika mambo mbalimbali ikiwemo sherehe, misiba na mikutano
ya siasa .
Jumla
ya wanachama waliojiunga katika wiki ya kilele cha sherehe hizo ni 1534
kati ya hao kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA ni 29 na Civic United
Front (CUF) 21
pia Chama hicho kimefanikiwa kuongeza idadi ya ofisi za kata hadi
kufikia 142, matawi 1120 na mashina 11100 lengo likiwa ni kusogeza
huduma karibu na wananchi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekezwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Lindi,Ndugu Adeline Gefi sehemu ya kupita ili kupokea maandamano ya wana CCM na wananchi wa mkoa huo wakati wa kilele cha sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho zilizofanyika katika Kata ya Likunja, wilayani Ruangwa tarehe 2.2.2014. Wa kwanza kulia ni Dr. Maua Daftari, Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Lindi.
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi waliofika kwenye sherehe za kilele za CCM kutimiza miaka 37 zilizofanyika kimkoa katika Kata ya Likunja, wilayani Ruangwa tarehe 2.2.2013
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akipokea maandamano ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa sherehe za kilele cha kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi mkoani humo zilizofanyika katika kata ya Likunja iliyoko katika wilaya ya Ruangwa tarehe 2.2.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua shina la wakereketwa la Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) katika Kata ya Likunja wakati wa kilele ya sherehe ya miaka 37 ya CCM zilizofanyika katika kata hiyo tarehe 2.2.2014. Mara baada ya kuzindua tawi hilo Mama Salma akapokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa viongozi wa UWT wa Kata hiyo na picha ya mwisho ikiwaonyesha akina mama wajumbe wa Tawi hilo wakishangilia baada ya uzinduzi huo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka Bibi Mwanahawa Ali, mjumbe wa UWT wa Kata ya Likunja kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Ruangwa wakati wa kilele cha sherehe za CCM kutimiza miaka 37.
Ngoma za utamaduni za makabila mbalimbali ya mkoa wa Lindi zilishamiri katika kilele cha sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Mkoani Lindi katika Kata ya Likunja huko wilayani Ruangwa. Hata muziki wa kizazi kipya nao uliporomoshwa katika kilele hicho. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe hizo

za utamaduni za makabila mbalimbali ya mkoa wa Lindi zilishamiri
katika kilele cha sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi
zilizofanyika Mkoani Lindi katika Kata ya Likunja huko wilayani
Ruangwa. Hata muziki wa kizazi kipya nao uliporomoshwa katika kilele
hicho. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa Mgeni Rasmi kwenye
sherehe hizo

sherehe hizoNgoma za utamaduni za makabila mbalimbali ya mkoa wa Lindi zilishamiri katika kilele cha sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika Mkoani Lindi katika Kata ya Likunja huko wilayani Ruangwa. Hata muziki wa kizazi kipya nao uliporomoshwa katika kilele hicho. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe hizo
Mmoja wa wana CCM akilishwa keki
Mgeni Rasmi katika kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi, Mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi katika sherehe zilizofanyika katika Kata ya Likunja, wilayani Ruangwa tarehe 2.2.2014.

Baadhi ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete wakati wa kilele cha sherehe za kutimiza miaka 37 ya chama hicho zilizofanyika katika kata ya Likunja, wilayani Ruangwa tarehe 2.2.2014.

Baadhi
ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi wakisikiliza hotuba ya mgeni
rasmi, Mama Salma Kikwete wakati wa kilele cha sherehe za kutimiza miaka
37 ya chama hicho zilizofanyika katika kata ya Likunja, wilayani
Ruangwa tarehe 2.2.2014. Picha zote na John Lukuwi
0 comments:
Post a Comment