Timu zikisalimiana
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu
ya Kagera Sugar wakiikaribisha timu ya Rhino Ranger leo kutoka Tabora
kwenye Ligi kuu ya Vodacom (VPL) wameifunga bao 1-0. katika mchezo huo
ulio pigwa hii leo jumamosi katika kipindi cha kwanza timu zote mbili
zilienda mapumziko zikiwa 0-0. Kipindi cha pili Kagera Sugar walifanya
mabadiliko kwa kumuingiza mchezaji wao Seleman Kibuta na katika dakika
ya 52 kipindi hicho hicho cha pili mchezaji huyo aliwapachikia bao la
pekee. Bao hilo limepatikana baada ya kupigwa frii kiki na Hussein
Mohamed(Shabalala) na kugonga posti upande wa juu na hatimaye Seleman
Kibuta kuumalizia mpira huo ndani ya lango la Rhino Rangers.
Bao
hilo limedumu mpaka dakika za mwisho wa kipute hicho na Kagera Sugar
kumaliza mtanange huo na ushindi wa pointi tatu muhimu kwenye uwanja wao
wa Nyumbani Kaitaba. Ushindi huu wa Kagera Sugar umewapandisha hadi
nafasi ya tano wakiwa na pointi 26 huku Rhino Rangers wakiendelea
kushika nafasi ya mwisho kwenye ligi hiyo wakiwa na pointi 13.
Picha ya waamuzi na timu kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mtanange kuanza
Viongozi wa timu ya Rhino Rangers pamoja na wachezaji wa akiba
Sehemu ya Kagera Sugar, Viongozi na wachezaji wa akiba
Kimbiza kimbiza
Nivute nikuvute!!!
Mchezaji wa Rhino akiuchota mpira kutoka kwa mchezaji wa Kagera Sugar
Patashika
kwenye lango la Kagera Sugar, Chupuchupu wafungwa ...Salum Kononi
ameuondosha mpira uliopigwa kichwa kabla haujavuka mstari ndani ya
lango.
Kanoni akimiliki mpira huku mchezaji wa Rhino akiwa amemnyemelea kwa nyuma!
Mchezaji wa Kagera Sugar akiwekwa chini...
katika kuwania mpira
Kagera Sugar wakifanya mabadiliko kipindi cha pili...
Seleman Kibuta akishangilia bao lake la pekee kwa timu yake Kagera Sugar katika kipindi cha pili dakika ya 52.
Kipa wa Rhino akiwapanga wachezaji wake wakati wa frii kiki iliyokuwa inaelekezwa kwenye lango lake.
Salum Kanoni akiwakimbiza Rhino Rangers
Wametwibia bao bwana..
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI MATUKIO BLOG
0 comments:
Post a Comment