Chelsea
imeonyesha mpira uko tofauti siku zote na wengi wanavyoamini kwa
kuichapa Man City kwa bao 1-0 ikiwa kwao Etihad jijini Manchester.
Bao
la Chelsea katika mchezo huo lilifungwa na beki wake wa kulia Branislav
Ivanovic ambaye aliukuta mpira unaelea baada ya Ramirez kupiga shuti
lililowababatiza mabeki wa Man City, naye akautupia kambani kiufundi
utafikiri mshambuliaji.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu
England iliyomalizika punde, kocha Jose Mourinho wa Chelsea ameingia
vyumbani haraka hata bila ya kumsalimia Pellegrini hali iliyoonyesha
kuwa amechanganyikiwa na furaha ya ushindi wa mechi hiyo.
Pamoja
na ushindi huo, Chelsea imeendelea kubaki katika nafasi ya tatu, ikiwa
na pointi 53 sawa na Man City lakini tofauti ya mabao ya kufunga na
kufungwa yanawabakiza vijana hao wa Manuel Pellegrini katika nafasi ya
pili.
Arsenal
ambayo jana iliichapa Crystal Palace inabaki katika nafasi ya kwanza
ikiwa na pointi 55, hivyo kufanya ushindani kuwa mkubwa zaidi kwa timu
tatu hizo ingawa Liverpool yenye pointi 47 si ya kuidharau.
Katika mechi ya leo, Chelsea ndiyo
ilipoteza nafasi nyingi huku ikionyesha soka tofauti la kushambulia kwa
‘kaunta atak’ tofauti na wengi walivyotarajia kuwa itapaki basi ili
kuzuia kasi ya upigaji mabao ya Man City.
Kama washambuliaji wa Chelsea
wangetulia kidogo tu, basi wangekuwa na uwezo wa kufunga hata mabao
mengine angalau mawili na kupata ushindi mzuri zaidi ya huo wa 1-0.
NA MAJJID MJENGWA
0 comments:
Post a Comment