Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kushoto ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Rished Bade.
Baadhi ya waandishi wa habari
waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum katika ukumbi
wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
--
Na Frank Mvungi
Serikali
imesema pato la Taifa limeendelea kukua kwa asiliamia 7 kwa mwaka
katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2013 kutokana na mikakati mizuri ya
maendeleo iliyotekelezwa kwa kuzingatia dira ya Taifa ya maendeleo.Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha Mh.Saada Mkuya Salum wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Saada
alibainisha kuwa katika robo ya tatu ya mwaka 2013 kiwango halisi cha
ukuaji wa uchumi kilikuwa asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 7.2
katika kipindi kama hicho cha mwaka 2012.
Katika
hatua nyingine Saada alisema kuwa Serikali imejipanga kuongeza pato kwa
ufanisi zaidi ili kuongeza pato la Taifa na kupunguza ukwepaji wa kodi
kwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi na kuwa ya kisasa zaidi.Aliongeza
kuwa Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) itaendelea kutoa
elimu ya matumizi ya mashine za kielektroniki ili kusaidia wananchi
kuelewa umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa.
Hata
hivyo alibainisha kuwa Serikali imekubaliana na wafanyabiashara kuwa
mwisho wa kuanza kutumia mashine za kielektroniki umesogezwa hadi tarehe
30 januari, 2014 ili kuwapa wananchi muda wa kujiandaa na kuanza
matumizi ya mashine hizo.
Pia
alitoa rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezaji
wa azma ya kuboresha mapato ya Serikali ili kuwaletea wananchi
maendeleo endeleo.
Wizara
ya Fedha imekuwa ikitimiza majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Taifa
ya Maendeleo 2025,Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini
(MKUKUTA) malengo ya maendeleo ya Milenia (MDGs) Ilani ya Uchaguzi mkuu
ya CCM ya mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment