Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya
umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu
Kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na
elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya
ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na
shule za msingi nchini.
Akizungumza
na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC),
Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi
kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi
yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni
muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na
sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi
ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku
ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya
maangamizi ya moto.
Alisisitiza
kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio
na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi
na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.
Nkhoma
amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au
rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu
wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
Wanafunzi
wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema
maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.
Wakati
huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya
kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi
ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti,
mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za
mwisho katika hali ya kinyama.
“Umoja
wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena,
lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica
inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema
taarifa hiyo.
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment