Marehemu Grace Kafumba
Familia ya Hayati Jenkins Kafumba wa Kanisa Road, Chang’ombe, Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mzazi, Mama Grace Kafumba kilichotokea asubuhi ya Ijumaa, Januari 3, 2014, katika Hospitali ya Tumaini mjini Dar es salaam.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Kanisa Road, Dar es Salaam.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote walioko Bagamoyo, Malawi, Canada, Uingereza, Afrika Kusini na popote pale walipo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina lake na lihimidiwe.
AMINA
0 comments:
Post a Comment