Cristiano Ronaldo amemtakia kheri mpinzani wake wa zamani Radamel Falcao apone haraka na kusema "soka inamhitaji Falcao" katika fainali zijazo za kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Monaco, hatocheza msimu mzima baada ya kupata maumivu makubwa ya goti mapema mwezi huu, na mpaka sasa hakuna uhakika wa kwenda kushiriki kwenye michuano ya dunia mwezi 6 mwaka huu.
Hata hivyo daktari ambaye amemfanyia opasuaji mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico amesema anaweza kupona mapema na kushiriki World Cup na Cristiano Ronaldo ana matumaini Falcao atapona na kurejea dimbani mapema.
"Ujumbe pekee ninaoweza kumpa ni kwamba ninajua ana nguvu sana na mjasiri mno, ninatumaini atapona haraka na arudi dimbani kwa sababu soka inamhitaji Falcao.
"Kombe la dunia na timu ya Colombia inamsubiri. Naomba apone haraka na kurudi kucheza. Ni kitu ambacho wote tunataka kama familia ya soka."
Falcaoalikuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa La Liga kabla hajajiunga na Monaco wakati wa kipindi cha kiangazi kilichopita na alikuwa na upinzani na Ronaldo mara kwa mara ukizingatia timu zao ni pinzani pia.
Na shaffihdauda.com

0 comments:
Post a Comment