SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, January 5, 2014

Kamati Kuu ya Chadema imeamua Kuwavua Rasmi Uanachama ndugu Samsoni Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo

 Aliyeakua Mwenyekiti Wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba
Dr. Kitila Mkumbo 
----
M/Kiti Taifa ameingia ofisini kwa Katibu Mkuu na muda wowote kuanzia hivi sasa M/Kiti atakuja kuzungumza na Waandishi wa Habari akiambatana na Ujumbe wa Wakurugenzi na Maofisa wa Chama.
Viongozi Wakuu akiwemo Katibu Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wameshawasili hapa na sasa Mh. John Mnyika ndio anawakaribisha Waandishi wa Habari na Kutoa salamu za utangulizi Mnyika anaanza kwa kuomba radhi kwa press kuchelewa anasema ni kwasababu ya uzito wa hoja zenyewe kwasababu Kamati Kuu iliiagiza Sekretarieti kuandaa tamko la leo. 

Pia Mnyika amewatambulisha Viongozi wa Kanda waliopo mahali. M/Kiti hayupo hapa mbele na badala yake Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa ndie anazungumza na Waandishi wa Habari na tayari ameshaanza kuzungumza Katibu Mkuu nae anaanza kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kuanza press akiungana na John Mnyika pia Katibu Mkuu anasema kuwa atasoma neno kwa neno kutokana na umuhimu wa hoja yenyewe! Ameanza kusoma na kusema kamati kuu ilikuwa ni ya dharura iliyokuwa na lengo la kuwajadili Wanachama watatu Dr. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na Samsoni Mwigamba.
Dr Slaa anaonyesha kabrasha lenye nyaraka mbalimbali ikiwemo mkakati wa mabadiliko 2013, mashtka ya watuhumiwa na nyaraka nyingine muhimu. Sasa Dr. Slaa anasoma mashtaka yote 11 ya Watuhumiwa kama walivyokabidhiwa kwa maandishi Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake.

Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.

Dr. Kitila Mkumbo alikataa kuzungumzia vifungu vya katiba walivyodai vimevunjwa kwa madai kuwa tayari wana malalamiko kwa msajili tayari. Aidha Dr. Kitila Mkumbo alishindwa kuithibitishia Kamati Kuu kwa ushahidi kuhusu madai ya taarifa ya fedha ambazo yeye na Zitto walishiriki, pia alishindwa kuonyesha ushiriki wa M/Kiti katika manunuzi ya vifaa mbalimbali vya Chama zikiwemo pikipiki za Chama.

Hivyo Kamati Kuu imeamua kuwavua Uanachama ndugu Samsoni Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo kuanzia tarehe ya jana baada ya maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu. Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.

Dr. Slaa anasema malengo ya waraka wa mabadiliko hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa Viongozi wa Chama.
 
Mwisho
Chama kinawatangazia Wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na Washirika wake kwa jina la Chama.

 Kuhusu madai ya Mwigamba juu ya kipengele cha Katiba Dr Slaa anaonyesha baraua ya tarehe 13 July 2006 iliyosainiwa na Ndugu Shaibu Akwilombe aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wakati huo kwenda kwa Viongozi wa Mikoa nchi nzima ambayo ilionyesha mabadiliko ya kipengele hicho pamoja na kipengele kilichomruhusu M/Kiti kuteua Manaibu Katibu Wakuu na Katibu Mkuu ambacho kwa makusudi hawakilalamikii kwasababu kilimnufaisha Zitto Kabwe.

Dr. Slaa anaongeza kuwa lengo la wakina Kitila lilikuwa ni kuonyesha kuwa CHADEMA na CCM ni walewale wote ni Mafisadi ili kukiharibia Chama sifa yake mbele ya Jamii. Dr. Slaa anasema Kamati Kuu imechukua maamuzi haya kwa uchungu kwasababu CHADEMA haina lengo la kupunguza wanachama bali kuongeza Wanachama hata wanaCCM katika kuharikisha ukombozi wa Taifa letu.

Dr. Slaa anamkaribisha Mh. Tundu Lissu ili kuongezea taarifa. Lissu anasema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009 alipokuwa akiwasiliana akina Denis Msack wa Mwananchi. 

Lissu anasema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya ugaidi ambapo katika mahojiano yake ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba zitto hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa Chadema imtose Wilfred Lwakatare.
Lissu anaongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari mawili ya Nimrod Mkono na Mkono mwenyewe ndie amewaambia taarifa hizo. Mkono amewaambia kuwa amempa Zitto hela nyingi sana na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod Mkono wakati Nimrod Mkono alikuwa ni namba sita katika orodha ya Mafisadi iliyotajwa pale Mwembeyanga.

Lissu anasisitiza kuwa washirika wa usaliti huu na uhaini huu hawakupenda kutangazwa kuwa wao ni Wasaliti na wahaini lakini yeye anasema wale ni Wahaini na Wasaliti. Lissu anasema kuwa Zitto anaendelea kuwa Mwanachama na Mbunge wa CHADEMA kwasababu ya Mahakama tu na sio kwasababu ya mapenzi ya CHADEMA.

Dr. Slaa anasoma mawasiliano kati ya Zitto na Mtu anayejiita Chadema Mpya. ambapo anasisitiza kuwa Mkakati ulianza kutekelezwa mapema kwa hiyo hoja kuwa Zitto alikuwa hajui Mkakati ni ya Uongo.

Mnyika anamalizia kwa kusema kuwa tuko katika vita dhidi ya maadui wa Chama walioko nje na ndani ya Chama. Hivyo falsafa yetu ya Nguvu ya Umma ndio itakayotusaidia kwa hiyo anatoa wito kwa Wanachama nchi nzima kuitumia falsafa hiyo katika hatua zote ili kushinda vita hii.

Pia anawaomba Wanachama wote kujitokeza kwa wingi mahakamani siku ya kesho katika kusikiliza maamuzi ya Mahakama. Press imeisha Asantheni kwa Kutufuatilia

*Update:Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari-Chadema  Muda:16:03.

0 comments:

Post a Comment