SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 10, 2013

TASWIRA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS:HITIMISHO LA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JANA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, jana usiku wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru, alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika kuhitimisha sherehe hizo. Kushoto kwake ni Rais wa Zanzibar, Dkt.  Mohamed Ali Shein na mkewe Bi Mwanamwema Shein.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Shein, wakifurahia burudani ya ngoma za asili iliyokuwa ikiendelea jukwaani wakati wa hitimisho la sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal na (kulia) ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Bi Mwanamwema Shein. 
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akiteta jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, wakati hitimisho la sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal na (kulia) ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Bi Mwanamwema Shein.
 Kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoa wa Katavi, kikitoa burudani jukwaani wakati wa sherehe hizo zilizohitimishwa kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam
Wasanii wa ngoma ya asili ya Kabila la Wahaya ‘Kakau Band’, wakitoa burudani jukwaani wakati wa sherehe hizo zilizohitimishwa kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments:

Post a Comment