Tunatua Salaam za Rambirambi kwa kifo cha Dada yetu mpendwa, Marehemu
Flora Komba kilichotokea siku ya Jumatatu Dec 30, 2013 huko Jijini
Seattle Washington Nchini Marekani.
Hayati alikua ni mwanaharakati wa kusaidia nyumbani kwa mfumo wa
kuthaminisha na kuwaenzi watoto yatima na wale ambao wanaoishi katika
mazingira magumu katika Wilaya ya Songea, mkoa wa Ruvuma, kusini mwa
Tanzania, huku akiukuliwa na ugonjwa mkali wa saratani uliyokuwa
ukimsumbua kwa siku nyingi wakati alipokua katika harakati za kukusanya
michango sehemu mbalimbali Jijini Seattle Wa, kwajili ya kupigania
kuleta maendele nchini Tanzania.
Marehemu katika harakati zake alikua akithamini sana watoto kupitia kupitia NGO kwenye tovuti ya The Mwangaza Foundation (hmwangazajitegemee.org/) pamoja na ukurasa wa Facebook page (facebook.com/pages/Mwangaza-Foundation/160059680720944)
ambapo alikua akiwashirikisha wengi kujumuika kuungana nae katika
kuleta maendeleo kusaidia watoto wanaokumbwa na matatizo ya malazi,
chakula, maji, elimu, huduma za afya na pia kuwa na upendo kwa watoto
wenye matatizo kama hayo.
Msimba wa Dada yetu mpendwa hayati Flora Kombani Msimba wetu sote
tunawaomba Tanzania wote wa Seattle, WA na vitongoji vyake kujumuika kwa
pamoja, kwa hali na mali kutoa mchango wao hadi pale atakapozikwa
Marehemu Msiba unaendelea nyumbani kwa marehemu.
Anuwani ni 13012 NE 121st Ln #J206
Kirkland, WA 98034
Mungu aiweke ROHO yake mahali pema Ameen !!!
SOURCE: SWAHILIVILLA
Angali video ya maelezo ya Mwangaza Jitegemee Foundation- Documentary
SOURCE: SWAHILIVILLA
Angali video ya maelezo ya Mwangaza Jitegemee Foundation- Documentary
0 comments:
Post a Comment