Aliyekua Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Mathayo
Aliyekua Waziri wa Ulinzi Shamsi Vuai Nahodha
Aliyekua Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki
----
Rais Jakaya Kikwete ametengua rasmi uteuzi wa Mawaziri wa nne
waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za
kiraia wakati wa Oparesheni Tokomeza Ujangili iliyokuwa ikiendeshwa na
Serikali.
Akisoma Bungeni mjini Dodoma jana jioni, Taarifa hiyo ya Rais, Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda Bungeni mjini Dodoma kuwa Rais ameridhia maoni ya
Wabunge wakati wa kujadili ripoti ya Kamati iliyoundwa na kuongozwa na
Mbunge James Lembeli kuwa Mawaziri waliotuhumiwa waondoke.
Mawaziri waliotakiwa kujiuzulu ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Balozi, Hamisi Kagasheki, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. John Nchimbi
pamoja na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo.
Lakini kabla ya kutanga taarifa hiyo Bungeni Waziri Kagasheki alitangaza rasmi kujiuzulu mbele ya Spika na Bunge.
Aidha Wabunge pia walimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda naye kujiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia mawaziri wake.
Kuenguliwa
kwa Mawaziri hao kumekuja baada ya Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe James Lembeli
kuwasilisha ripiti ya kamati yake na kujadiliwa kwa kina Bungeni hii
leo.
Lembeli amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti
ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya
kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama.
Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa
wafugaji wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na
pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.
Msikilize Aliyekua Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kagasheki akitangaza Kujiuzulu
Sikiliza
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisoma Taarifa ya Rais Jakaya Kikwete
Bungeni mjini Dodoma ya kuridhia maoni ya Wabunge wakati wa kujadili
ripoti ya Kamati iliyoundwa na kuongozwa na Mbunge James Lembeli kuwa
Mawaziri waliotuhumiwa wajiuzulu.
Hitimisho la Waziri Mkuu Mizengo Pinda
0 comments:
Post a Comment