SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, December 7, 2013

MAKAMU WA RAIS ASAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU KUFUATIA KIFO CHA MZEE MADIBA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Afrika ya Kusini Masaki  jijini Dar es salaam leo Disemba 6-2013, kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela (95) aliyefariki Dunia jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg. kushoto ni Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Henry Thanduyise Chilize.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi na Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania Henry Thanduyise Chiliza kwenye ofisi ya Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini Dar es salaam leo Disemba 6-2013, wakati alipofika kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela (95) kilichotokea jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania Henry Thanduyise Chiliza kwenye ofisi ya Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini Dar es salaam leo Disemba 6-2013, wakati alipofika kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela (95) kilichotokea jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments:

Post a Comment