Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiifungua rasmi
tafrija ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
katika Ukumbi wa Mtenda Sunset mara baada ya kikao cha baraza kilichokuwa
kinafanyika kwa siku tatu katika Hoteli
ya Paradise jijini Mbeya. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,
Mwamini Malemi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati) akiwaongoza
watumishi wengine wa wizara wake kusakata rumba katika Ukumbi wa Mtenda Sunset
baada ya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo cha siku tatu kufungwa katika
Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Wanne kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Mwamini Malemi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa
(kushoto) akisakata rumba katika miondoko ya twisti na Mkurugenzi Msaidizi wa
wizara hiyo, Nigel Msangi katika Ukumbi wa Mtenda Sunset baada ya Kikao cha
Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo cha siku tatu kufungwa katika Hoteli ya
Paradise jijini Mbeya. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakisakata rumba katika Ukumbi wa Mtenda
Sunset huku wengine wakiwaangalia wanavyosakata rumba baada ya Kikao cha Baraza
la Wafanyakazi wa wizara hiyo cha siku tatu kufungwa katika Hoteli ya Paradise
jijini Mbeya.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment