SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, November 24, 2013

MAHAFALI YA NNE YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) YAFANA LEO KATIKA VIWANJA VYA CHIMWAGA

 Bendi ya Jeshi la Wananchi likiongoza masafara wa elimu kuelekea katika viwanja vya Chimwaga kwaajili ya Mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyohitimishwa leo kwa Wahitimu Mbalimbali kutunukiwa Shahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Benjamin Mkapa.
 Msafara wa Elimu ukienda kwenye Viwanja Vya mahafali leo, mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyohitimishwa leo katika Viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idrisa Kikula (Mbele) akiongozana na Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Benjamin Mkapa (katikati) na Mkuu wa Baraza la Bodi ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Balozi Juma Mwapachu (kulia) leo katika mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyohitimishwa katika Viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo


 Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Benjamin Mkapa Wakiwa wamesimama Kwaajili ya Kuimba Wimbo wa Taifa kabla ya sherehe ya Mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kuanza


 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula Akitoa hotuba fupi kabla hajamkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kuongea machache kabla na yeye Kumakaribisha Mkuu wa Chuo Kwaajili ya Kuanza zoezi la kuwatunuku wahitimu wa shahada mbalimbali za Chuo Kikuu Cha Dodoma leo katika mahafali ya nne ya UDOM yaliyofanyika katika Viwanja vya Chimwaga


 baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali za Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakisubiri Mahafali yao ya Nne Kwaajili ya Kutunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo.


 Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Balozi Juma Mwapachu akisoma risala fupi kabla ya Kumkaribisha Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Benjamin Mkapa kuanza zoezi la Kuwatunuku wahitimu wa shahada mbalimbali za Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo katika mahafali ya Nne ya Chuo hiko yaliyofanyika leo katika Viwanja Vya Chimwaga


Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wa wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa nje ya Ukumbi wa Chimwaga Kabla ya Mahafali kuanza


Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wa wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakisubiri kushuhudia mahafali ya nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyomalizika leo tarehe 23 Novemba 2013 katika Viwanja vya Chimwaga Vilivyopo Chuoni Hapo



Ulinzi ukiimarishwa kila sehemu hapo askari wa JKT na Jeshi la polisi wakiwakagua ndugu,jamaa na marafiki wa wahitimu wa Shahada mbalimbali za Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika viwanja vya Chimwaga leo Kushuhudia ndugu zao wakitunukiwa shahada zao.
PICHA ZOTE NA JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG

0 comments:

Post a Comment