Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa Akiwa nje ya Ofisi ya Gavana wa Alabama
Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa
kwenye picha ya pamoja na gavana
Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa
akikaribishwa na Gavana
Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa Akiongea na Uongozi wa Jimbo la Alabama
Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa akiwa kwenye kikao
Uongozi wa jimbo na Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake
Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa akimshukuru mmoja wa askari waliokuwa wakiongoza msafara wake.Picha na Chadema
---
Katibu mkuu
wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini Marekani
iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza mambo
mbali mbali, imemfikisha jana katika jimbo la Alabama na kupokelewa na
wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara.
Alabama ni
moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo siku za
nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25 iliyopita,
viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la
Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari kama
Honda, Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station,
Wallgreens na mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.
Kupitia kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr.
Slaa alipata kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza
mbinu ambayo ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na
umasikini. Licha ya yote, Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake,
wako tayari kushirikiana na Tanzania kwenye mambo ya biashara hasa
miundombinu ikiwemo bandari, ujenzi wa madaraja na bandari. Dr. Slaa na
mkewe Josephine walipokelewa na Gavana pamoja na mawaziri wake.
Kubwa ya
yote alichojifunza Dr. Slaa ni kwamba, serikali inaweza kuwa na ufanisi
hata ikiwa na baraza dogo. Jimbo la Alabama lina Mawaziri sita tu, huku
CCM ikiwapa walipa kodi wa tanzania mawaziri 70 wasiokuwa na kazi. Wengi
wao wakiwa na matumizi makubwa huku wakina mama wakijifungua sakafuni,
walimu wakinyimwa haki zao, polisi na wanajeshi wakiishi hali duni na
wanafunzi wakisoma chini ya miembe. CCM ni janga kubwa lililowakumba
watanzania
Chuo Kikuu Cha Kilimo Auburn
Kadhalika
Dr. Slaa ametembelea chuo kikuu cha auburn ambayo ni moja ya vyuo vikuu
vikubwa zaidi vya utafiti duniani. Auburn Inafanya shuguli zake nchini
Kenya, Uganda, Senegal na kwingineko barani Afrika. Nchini Kenya, chuo
cha auburn inawasaidia wakulima mbalimbali hasa wafugaji wa samaki na
technologia za kisasa inayowawezesha kusafirisha samaki wengi kwenda
ulaya Ulaya. Kati ya Kenya na Uganda, utafiti wao umetoa zaidi ya ajira
7000.
Walipoulizwa
kwa nini walikwepa Tanzania, hawakuficha ukweli. Walinena kwamba ni
vigumu sana kufanya kazi Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa wangekuja na
fedha zao kutoka benki ya dunia na shirika la kimarekani la USAID
ambayo inadhamini miradi yao sehemu nyingi barani Afrika ikiwemo Kenya
na Uganda. Viongozi wa chuo hicho wako tayari kurudi Tanzania ikiwa
mazingira ya kazi yatabadilika hasa kukiwepo na serikali mbadala, ambayo
Mh. Slaa amewahakikishia kwamba Chadema hiko tayari kufanya nao kazi.
Viongozi wa
Auburn University wako tayari kusaidia vyuo vya Tanzania kama Sokoine
kwa kuwafundisha waalimu na pia kubadilishana nao technolojia za kisasa
za kilimo. Wako pia tayari kuwafundisha wakulima wa aina zote na hata
walaji mbali mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment