Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ( kushoto ) akiwa na Balozi wa kuwatetea
watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka
(10) Zuriel Oduwole, kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni
jijini Dares Salaam.
Balozi
wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye
umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole (kushoto) akipokelewa na Msaidizi wa
Rais katika masuala ya jamii Mwanahamisi Kitogo (kulia) kwenye ofisi
za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada ya kuitembelea
ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ( kulia) akisalimiana na Balozi wa kuwatetea
watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka
(10) Zuriel Oduwole (kushoto) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni
jijini Dares Salaam.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ( kulia) akizungumza na mama mzazi wa Balozi
wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye
umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole, Partricia Oduwole (kushoto) kwenye
ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada
kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini jijini Dares Salaam.
Aliyebebwa ni Ismachiah mdogo wake na Zuriel.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ( katikati) akiwa na Balozi wa kuwatetea
watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka
(10) Zuriel Oduwole(kulia ) wengine aliyevaa nguo ya njano ni Azaliah
na pinki ni Arielle ambao ni wadogo zake na Zuriel, kwenye ofisi za
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea ofisi
hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo kwa Balozi wa kuwatetea
watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka
(10) Zuriel Oduwole, kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo(WAMA) mara baada kuitembelea jana jioni jijini Dares
Salaam.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimwonesha tisheti yenye nembo ya Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Balozi wa kuwatetea watoto wa kike
kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel
mara baada kuitembelea ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares
Salaam.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimvalisha tisheti yenye nembo ya Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Balozi wa kuwatetea watoto wa kike
kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel
Oduwole ikiwa ni ishara ya kumteua kuwa balozi wa WAMA, alipoitembelea
ofisi hiyo hivi karibuni jijini Dares Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa
uboreshaji afya – WAMA Dk. Sarah Maongezi .
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimwonesha khanga iliyobuniwa na Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Balozi wa kuwatetea watoto wa kike
kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel yenye
maandishi ya ‘mtoto wa mwenzio ni mwanao mkinge na ukimwi’ kwenye
ofisi za mara baada kuitembelea ofisi hiyo jana jioni jijini Dares
Salaam.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimuonyesha Balozi wa kuwatetea watoto wa
kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel
Oduwole kinyago kinachoonyesha umoja wa watanzania wakati balozi huo
alipozitembelea ofisi za WAMA hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Picha
na Magreth Kinabo - Maelezo.
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
MKE wa
Rais Mama Salma Kikwete , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo (WAMA) amemtunuku Balozi wa kuwatetea watoto wa
kike katika masuala ya elimu kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye
umri wa miaka (10) Zuriel Oduwole kuwa mwanachama (balozi) wa heshima
wa taasisi hiyo.
Kauli
hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mama Kikwete mara baada ya Zuriel
kuitembelea ofisi ya WAMA iliyoko Ikulu jijini Dares Salaam na kufanya
mazungumzo kuhusu shughuli inazozifanya .
Mama
Kikwete alimwezea Zuriel jinsi taasisi yake inavyofanya kazi mbalimbali
ikiwemo ya kuhakikisha watoto wa kike yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi wanapata elimu ili waweze kuajiriwa na kujiajiri
ikiwa ni hatua ya kuendeleza maisha yao ya baade na kutimiza ndoto zao.
Kwa
mujibu wa baba wa Zuriel, Ademola Oduwole alisema mtoto wake pia
amekuwa akihamasisha wasichana kubadili mtazamo wa Bara la Afrika kwa
kuwa huko Marekani watu hawalijuwi bara hilo na wanadhani ni bara la
njaa .
“Amezindua
mradi wa dreaming up dreaming big' lengo lake ni kuwahamasisha watoto
wa kike kuwa na ndoto za kuendelea,” alisema Oduwole.
Oduwole aliongeza kuwa Zuriel anapenda kuhamasisha kuhusu suala la elimu kwa kuwa ndio njia ya kufikia malengo ya milinea.
Alisema
Zuriel ameshatembelea nchi Nigeria,Malawi na Tanzania ambapo alifika
Shule ya Msingi ya Olympio na Shule ya Sekondari ya Jangwani na Shule
ya Sekondari ya wasichana ya Marian.Pia ameshafanya mahojiano na
marais wanane wa Afrika , ambao ni wa Tanzania, Mauritius,
Kenya,Nigeria, Cape Verde,Sudan ya Kusini na Liberia.
Kwa
upande wake Mama Kikwete alifurahishwa na juhudi za Zuriel na kumtaka
kuendelea kufanya mambo makubwa katika kutimiza ndoto zake.
Naye Zuriel alishukuru kwa ukarimu alioupata kwa Watanzania na ameaihidi kuitangaza Tanzania na WAMA mahali popote duniani.
Zuriel
alikuwepo nchini kwa kipindi cha siku sita kuanzia jumapili iliyopita
akiwa na wazazi wake na wadogo zake Azaliah Arielle na Ismachiah,
amerejea Marekani mwishoni mwa wiki hii.
CHANZO: MICHUZI MATUKIO BOG
CHANZO: MICHUZI MATUKIO BOG
0 comments:
Post a Comment