Waziri
Mkuu Mstaafu, Mhe. John Samuel Malecela akisisitiza jambo wakati
alipokuwa akibadilishana mawazo na Baadhi ya maafisa wa Uwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ( hawapo pichani) na
wajumbe wanaohudhuria mikutano ya Kamati Kuu Sita za Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa. Mhe. Malecela ambaye yuko Jijiji New York kwa ziara
binafsi, alisisitiza sana umuhimu wa watanzania wote bila ya kujali
itikadi na tofauti za kisiasa, kuhakikisha wanaulinda mtaji wao mkubwa
ambao ni amani.
Muwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na
Mkewe Upendo wakifuatilia mazungumzo hayo ambayo yalifanyika katika
makazi ya Balozi , mazungumzo yaliyoambatana na chakula cha jioni.
Mke wa
Mhe. Malecelea, Mhe. Ann Kilango akifurahia jambo pembeni ni Naibu
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi
Ramadhan Mwinyi.
Mama Upendo Manongi mke wa Balozi Manongi akiwakarisha wageni wake chakula cha jioni.
Balozi Mwinyi, Balozi Mushy na Kanali Masalla nao wakipata chochote kitu.
Balozi Manongi akiwa na baadhi ya maafisa wake wakiendelea kujipakulia maakuli.
wakipata chakula.
Mhe.
Waziri Mkuu Mstaafu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa
wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Mhe. Waziri Mkuu Mstaafu akiwa na baadhi ya wajumbe wanaoshiriki mikutano mbalimbali inayoendelea hapa Umoja wa Mataifa
Na Mwandishi Maalum
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. John Samue Malecela ameeleza kwamba, hakuna mtaji mkubwa ambao watanzania wanauhitaji kama amani.
Ameyasema
hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokutana na kubadilishana mawazo na
maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, pamoja na wajumbe wanaohudhuria mikutano inayoendelea ya
Kamati Kuu Sita za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mazungumzo
hayo yaliyoambatana na chakula cha jioni yalifanyika katika Makazi ya
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi
“
Naomba niliseme hili, ninasema hivi , hakuna mtaji mkubwa tunaouhitaji
watanzania wote bila ya kujali itikadi wala tofauti zetu za kisiasa
kama amani” akasema Mhe. Malecela .
Na
kuongeza. “Nchi yetu inaoutajiri usioelezeka, hakuna wilaya isiyokuwa na
utajiri kuanzia gesi, madini ya kila aina, ikiwani madini ya namna
ya urani hadi makaa ya mawe, nchi yetu ni tajiri sana. Tunahitaji mitaji
ya kuendeleza utajiri huu. Lakini nasisitiza sana utajiri huu
tulionao hautakuwa na maana yoyote kwetu watanzania kama hatutadumisha
amani, upendo, mshikamano na uzalendo”.
Waziri Mkuu mstaafu na ambaye amefuata na mkewe Mama Ann Kilango yupo jijini New York kwa ziara binafsi.
Akasema
uchimbaji wa gesi ukianza na uchimbaji wa madini ya urani ukianza,
pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo inayoendelea hivi sasa, basi
miaka kumi ijayo Tanzania itapiga hatua kubwa sana za kiuchumi na
kimaendeleo.
Katika
mazungumzo hayo Mhe. Malecela licha ya kuzungumzia umuhimu wa amani
na matumizi mazuri ya raslimali , pia alizungumzia mafanikio na
changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa hivi sasa.
Kwa
upande wa maendeleo hakusita kuzungumzia mpango wa serikali wa kuwa na
shule za sekondari kila kata na kusisitiza kwamba ingawa uamuzi huo
umekuwa ukipingwa au kulalamikiwa na baadhi ya watu lakini ni mpango
ambazo umewapatia fursa vijana wengi ya kupata elimu ya sekondari na
matunda yake yanaonekana.
Kwa
upande wa ujenzi wa miundo mbinu na hususani barabara, Mhe. John
Malecela, amesema Serikali ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete inafanya
kazi kubwa na nzuri ya kuendeleza ujenzi wa mitandao ya barabara nchi
nzima.
“
Kusema ukweli, Mhe. Kikwete anajitahidi sana katika eneo hili hakuna
nchi katika eneo la Afrika Mashariki ambayo inaweza kushindana nasi
kwa upande wa barabara.” Akasema Mhe. Malecela
Na
kuongeza serikali haijaishia katika ujenzi wa barabara lakini pia
inaendelea na jukumu uimarishaji wa reli,ujenzi na upanuzi wa bandari
ukiwamo ujenzi wa bandari mpya katika eneo la Bagamoyo. Bandari
aliyoieleza kwamba itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuegesha meli
kubwa na zenye uwezo wa kubeba tani nyingi za mizigo.
Akizungumzia
uzefu wake katika tasnia ya diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe, John Malecela ambaye pia ni mwanadiplomasia mkomavu aliwataka
maafisa hao kutoyumba pale inapobidi kutetea misimamo na maslahi ya
nchi yao.
“ kwa
kweli ninawaonea huruma sana Mabalozi wa wakati huu, mnafanya kazi
katika mazingira magumu sana, enzi zetu nakumbuka nikiwa hapa Umoja wa
Mataifa miaka michache baada ya kupata uhuru Balozi ulikuwa na nguvu ya
kusimama kwenye majukwaa ya kimataifa na kutetea jambo bila ya
kuwaogopa wakubwa”. Akasema.
Na
kuongeza, “ Kuna mkutano mmoja nilitoa maneno makali dhidi ya Balozi
wa Israel wakati ule. Baada ya mkutano ule, Balozi yule alikuja
ofisini kwangu na kuniambia maneno yale niliyoyasema hayakuwa msimamo
wa nchi yangu”.
“
Lakini pia niliitwa nyumbani na Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere.
akaniambia John umezungumza nini huko, taratibu hao ni wakubwa na mimi
nikamjibu, Mhe. Rais naamini nimekuwakilisha vizuri. Ninachotaka
kusisitiza ni kwamba msiogope kutetea maslahi ya nchi yetu licha ya
changamoto za diplomasia za nyakati hizi”. Akasisitiza
0 comments:
Post a Comment