SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, September 29, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/09/DSC002651.jpg
DIWANI ATHUMANI – ACP -KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 29. 09. 2013.
WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO UTENGULE WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. JIDAYI S/O JINGAZA, MSUKUMA,   MIAKA 26, MKULIMA, NA MKAZI WA UTENGULE ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA
AFYA IGURUSI BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA NA FIMBO KICHWANI NA WATUHUMIWA  WANNE AMBAO NI {1} DONGEA S/O INAMBILI {2} KAMTIMBO S/O INAMBILI {3} INAMBILI S/O INAMBILI NA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE  BADO HAJAFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI NI UGOMVI ULITOKANA NA WATUHUMIWA KUTAKA KUMBAKA DADA WA MAREHEMU, WATUHUMIWA WAMETOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA  WALIYOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:45 HRS HUKO MASHALA IGURUSI BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI NO T.274 AUA AINA YA SUZUKI ESCUDO LIKIENDESHWA NA   DEREVA JOHN S/O MSHONGO. MIAKA 38, MPARE , DAKTARI, NA MKAZI WA FOREST MBEYA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE OBED S/O DONARD, MIAKA 32, MBENA, MKAZI WA MASHALA NA KUSABABISHA  KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA TARATIBU ZA MAZISHI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO MLOWO BARABARA YA MLOWO/KAMSAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI NO T.372 BYD AINA YA  T/NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA DAVID S/O ALEXANDER  @ MWAIPUNGU, MIAKA 30, MNYAKYUSA, MKAZI WA MLOWO LILIMNGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE SHUKURANI S/O MBEMBELA, MIAKA 32, MNDALI, DEREVA WA PIKIPIKI{BODABODA} NA MKAZI WA MLOWO  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA  SERIKALI VWAWA – MBOZI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KA
MISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by: [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

CHANZO MBEYA YETU BLOG

0 comments:

Post a Comment