Mkurugenzi
wa mawasiliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa
uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na British Council
utakaowawezesha walimu na wanafunzi kupata nafasi adhimu ya kujifunza
kupitia mfumo wa digitali kwenye shule zao. Mradi huo utashirikisha
shule za sekondari katika mikoa mbalimbali nchini. Pichani kushoto ni
Meneja huduma za jamii Hawa Bayumi , Kulia ni Mkurugenzi wa British
Council Tanzania Bw. Richard Sunderland leo
Mkurugenzi wa British Council Tanzania bwana Richard Sunderland akiongea wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na British council utakaowawezesha walimu na wanafunzi kupata nafasi adhimu ya kujifunza kupitia mfumo wa digitali kwenye shule zao. Mradi huo utashirikisha shule za sekondari katika mikoa mbalimbali nchini.Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya , kulia ni meneja mradi British Council Tanzania BiLilian Msuya.

ZAIDI
ya walimu na wanafunzi 25,000 kutoka mikoa tisa nchini wanatarajia
kupata nafasi adhimu ya kujifunza kupitia mfumo wa digitali kwenye shule
zao. Hii inatokana na ushirikiano kati ya Airtel na British Council
kutanua nafasi ya kunufaika na huduma inayotolewa na Airtel ya
kuunganishiwa 5GB za internet kwa mwezi katika mpango wa miaka mitatu
kwenye vituo 22 vya mfano wa matumizi ya digitali vilivyopo katika shule
mbalimbali nchini.
Kampuni ya
Airtel itaunganisha huduma ya internet kwenye vituo vya British Council,
shule hizo na jamii inayozizunguka. Vituo hivyo vya digitali tayari
vimekwishaandaliwa kupitia shirikiano na Microsoft huko Arusha,
Bagamoyo, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Dodoma, Zanzibar na Mara.
Kasi ya ajabu ya upatikanaji wa internet kwenye maeneo hayo kutoka
Airtel unawahakikishia walimu na wanafunzi fursa ya kupata elimu isiyo
na kikomo. Vituo hivyo kwenye shule zilizochaguliwa ni sawa na vituo vya
TEKNOHAMA (ICT) kwa walimu, wanafunzi na wakazi wa maeneo husika.
Kwa miaka
mitatu iliyopita, mamia ya wanafunzi nchini wamenufaika na mpango wa
British Council wa kuwaboreshea watoa elimu mchakato wa kujifunza na
kufundisha kwa kupitia TEKNOHAMA. Ni nia ya British Council kusapoti
matumizi ya TEKNOHAMA katika shule za Afrika kuwa endelevu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzinduliwa kwa ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Mr. Sunil Colaso alisema:
"Airtel
inaamini katika kuiwezesha jamii kupitia elimu, na leo tunajivunia
kupata nafasi ya kushirikiana na British Council katika juhudi za
kuikuza sekta ya elimu kupitia TEKNOHAMA," na kuongeza:
"kutokana na kukua kwa sekta ya TEKNOHAMA katika dunia ya kisasa, ni muhimu sana kuwapa ujuzi watoto wetu wakiwa katika umri mdogo."
"kutokana na kukua kwa sekta ya TEKNOHAMA katika dunia ya kisasa, ni muhimu sana kuwapa ujuzi watoto wetu wakiwa katika umri mdogo."
Mkurugenzi wa British Council nchini, Bw. Richard Sunderland, alisema:
"Ushirikiano huu na Airtel unajenga na kuimarisha kile kinachojulikana kama 'Badiliko partnership' kati ya British Council na Microsoft, umoja unaolenga kusambazwa kwa TEKNOHAMA kwenye shule mbalimbali nchini," akaongeza: "ni ushirikiano utakaoboresha ubora wa maisha ya jamii kwa njia ya uwajabikaji wa makampuni kwa jamii (corporate social
responsibility) kupitia elimu."

British
Council imewekeza katika ushirikishwaji wa kidigitali unaoziwezesha
shule za Afrika kushirika katika ubadilishanaji wa maarifa na mawazo
duniani. TEKNOHAMA iliyoboreshwa huwawezesha walimu kuyaunganisha
madarasa yao na mengine popote duniani, hivyo kuwapa wanafunzi kitu
kipya kimataifa na kuwa na utambuzi mpana. Katika kuunga mkono juhudi za
serikali kwenye eneo hilo, British Council imeandaa warsha maalumu ya
kuzungumzia sera kwenye nchi mbalimbali kuizungumzia hilo, na hapa
nchini warsha hiyo itafanyika mwezi ujaoBritish Council
0 comments:
Post a Comment