SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 4, 2013

Wamiliki Wa Shule Waipongeza Serikali

Kitendo cha matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kuonyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo walipata sifuri kiliwachanganya wamiliki wa shule nchini ambao jana waliibuka na kuipongeza Serikali kwa kufuta matokeo hayo na kuamuru mitihani isahihishwe upya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, Kwa upande wake, Mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Giftskillful iliyopo Kibaha Mwendapole, Miriam Kilamiani aliipongeza Serikali kwa hatua hiyo iliyochukua na kusisitiza kuwa yalifanyika makosa katika usahihishaji.

“Haikuwa sahihi kueleza kuwa wastani wa ufaulu umepanda bila kuwaandaa wanafunzi, binafsi matokeo ya wanafunzi wangu sikuyaamini kwa kuwa nilijua wazi uwezo wao haukuwa hivyo,” alisema Kilamiani.

Alisema anaamini kuwa uamuzi wa serikali kufuta matokeo hayo na kuagiza Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) kuyaandaa upya kutaifanya shule yake kupata matokeo stahiki.

Mmiliki huyo wa shule alieleza kwamba mbali na kuwa na mitalaa ya aina moja, kila jambo linalobadilika katika sekta ya elimu wadau wote wanatakiwa kuelezwa ili watoe ushauri na kujipanga jinsi ya kukabiliana na mabadiliko hayo.

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Green Acres, Julian Bujugo alisema uamuzi wa Serikali ni mzuri na akapendekeza kufukuzwa kazi kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Joyce Ndalichako kwa kuwa katika uongozi wake, matokeo yamekuwa na utata mkubwa.

“Haki imetendeka na kilio chetu kimesikika, Necta wakati inatoa matokeo yake inatakiwa kuzingatia maendeleo ya wanafunzi katika mitihani yote ukiwamo wa moko” alisema na kuongeza;

“Zamani walikuwa na utaratibu wa kukutana na viongozi wa shule kabla ya kufanyika kwa mitihani lakini hivi sasa haipo hivyo. Pia iwepo mitalaa inayofanana kwa shule zote nchini.”

Alisema Ndalichako anatakiwa kujiuzulu kwa kuwa katika uongozi wake kumekuwa na utata mkubwa katika matokeo ya mitihani mbalimbali, kwamba hilo limedhihirika baada ya Serikali kuamua kufuta matokeo hayo.
kukabiliana na mabadiliko hayo.
CHANZO: HIKI HAPA

0 comments:

Post a Comment