Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akisisitiza jambo, wakati alipokuwa akikifungua kikao cha Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Machano Khamis Ali na kulia Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani.
Anaripotiwa kusema nyongeza ya miaka 2 baadaya mwaka 2017, inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa uchaguzi kufanyika mwaka 2015.
Gazeti la Mwananchi linasema madai hayo ya yamepingwa vikali na Serikali na viongozi wake watatu waandamizi walipoulizwa kwa maandishi na mwandishi mjini Dodoma:
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alijibu: “Mchakato wa Katiba upo ‘on track’ (unakwenda vizuri) hatuna sababu ya kufanya hivyo.”
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijibu” “Njooni ofisini kwangu nitasema ni kitu gani.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alijibu kwa utani bila ya kufafanua: “Njooni niwajuze, unajua kamba haitoki Ukambani kama ilivyo kamba.”
Profesa Lipumba amemwomba Rais Kikwete asilikubali wazo hilo: "Nitapenda kuona Rais Kikwete akikataa jambo hilo kwani litachafua taswira ya nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala bora." na kusisitiza kuwa Serikali haipaswi kuhofia uchaguzi kwa sababu ya Katiba kwani bado uwezekano wa kuandaa uchaguzi wa haki na huru unawezekana kwa utaratibu mwingine: aMchakato wa Katiba unaendelea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatuambia kwamba mwaka 2014 tutakuwa na Katiba Mpya, sasa CUF tunasema kwamba hata kama Katiba Mpya haitapatikana kwa kipindi hicho kuwe na Tume huru ya Uchaguzi."
JUKATA Latimkia Mahakamani
Wakati hayo yakijiri, Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), limesema lina mpango wa kufungua kesi mahakamani ili mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba Moya isitishwe kutokana na kuwepo kwa manung'uniko kadha wa kadha kuhusu uendeshwaji wake, tuhuma za rushwa, mwingiliano wa itikadi za vyama n.k.
Deus Kibamba, Mwenyekiti wa JUKATA amekaririwa akisema kuwa ndani ya siku 7 zijazo (hesabu uanzia jana Mei 14, 2013), jopo la Mawakili wake 10 wakiongozwa na Dk Rugemeleza Nshala litawasilisha mahakamani hoja 5 zifuatazo:
Source: WAVUTI
0 comments:
Post a Comment