Rais Jakaya Kikwete
****
Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za
ufunguzi wa barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango
cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Aidha, sherehe hizo
zitahudhuriwa na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Changamoto za Milenia wa Marekani.
Barabara
ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na
nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa
Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium
Challenge Corporation – MCC).
Kukamilika
kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya
kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika
kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya
na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Sherehe hizi zitafanyikia kijiji cha Kisera katika Wilaya ya Nkinga mkoani Tanga.
Taarifa hii imetolewa na;
Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU
0 comments:
Post a Comment