SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 11, 2012

RAYC Amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, Amshukuru Kwa Msaada Wa Matibabu.



http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/RAY-C-akimishukur-Rais-Kikwete.jpg
RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/RAY-na-Mamama-na-Dada-yake-ikulu.jpg
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.
 (picha na Freddy Maro).
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, jana mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012

0 comments:

Post a Comment