SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 11, 2012

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU KWA KAULI MBIU YA “Sauti yangu inachangia

Mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kusalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot.
Pichani Juu na Chini ni maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali, Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
 
Meza Kuu ikipokea maandamano ya Wanafunzi na Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali wakati sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu zilizofanyika jijini Dar leo.

SHEREHE YA MIAKA 7 YA THT FUNIKA BOVU NDANI YA DAR LIVE

Familia ya THT ikiwa jukwaani wakati wa kusherehekea miaka 7 toka kuanzishwa.
Shilole na kundi lake wakilishambulia jukwaa la Dar Live.
Vijana wa THT wakiwasha moto wakati wa sherehe yao ya kutimiza miaka 7 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Kambi Popote ya Clouds Tv Kuungana na Lakeland Africa Safari ya Siku 14 za ‘Mtanzania Tembelea Tanzania’ Kukuza Utalii wa Ndani.

 http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/31.jpg
Kipindi cha Kambi Popote kinachorushwa Clouds Tv kitaungana na Lakeland Africa kwenye safari ya siku 14 za ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ amabyo itaanza desemba 14 mwaka huu na kumalizika desemba 27 mwaka huu.

Mtangazaji wa kipindi hiki Antonio Nugaz ataiongoza timu yake nzima katika safari hii ya kuvutia huku timu yote kwa ujumla ikipata huduma ya tour guide maarufu kutoka Lakeland Africa mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 3o katika sekta ya utalii.

Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Olduvai Gorge, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Watanzania watakaosafiri na Kampuni ya Lakeland Africa katika safari hii ya siku 14 za ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ watapata huduma safi ndani ya lori la kitalii wakiwa safarini ikiwemo kila mtalii kuwa na soketi yake ya kuchajia simu, laptop na kamera.

Pia kila mtalii atakuwa na kabati lake dogo (locker) kwa ajili ya kufungia vitu vyake vya thamani kama vile passport, vitambulisho na kwamba kila mtalii anatakiwa kuja na kufuli lake la kufungia kabati lake.

Mbali na hayo kila mtalii atakuwa na taa yake ya kusomea wakati wa usiku, gari lina tanki la maji lenye ujazo wa lita 500 na kila mtalii atapewa lita 20 kwa siku na kwamba kutakuwa na firiji ya vinywani baridi na vitu vinavyoharibika.

Kwa mawasiliano na Lakeland Africa

+255222-761811

+255784885901

Email: reservations@lakelandafrica.com

‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’

RAYC Amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, Amshukuru Kwa Msaada Wa Matibabu.



http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/RAY-C-akimishukur-Rais-Kikwete.jpg
RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/RAY-na-Mamama-na-Dada-yake-ikulu.jpg
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.
 (picha na Freddy Maro).
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, jana mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012

Mazungumzo baina ya Serikali ya DRC na waasi wa M23 yanaendelea jijini Kampala.

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/12/drc.jpg
Mazungumzo baina ya ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pamoja na waasi wa kundi la M23 yameanza yanaendelea mjini Kampala Uganda, chini ya usuluhishi wa mwenyekiti wa nchi za kanda ya maziwa makuu. Mazungumzo hayo yameendelea, licha ya mkasa uliotokea juzi, baada ya ujumbe wa waasi kuilaumu serikali ya Kongo kuwa inawafadhili waasi kutoka nchi jirani na walio tishio kwa usalama wa nchi hizo pamoja na raia wa mashariki mwa Kongo.