SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 2, 2012

ZUNGU AKANUSHA KUKAMATWA NA RUSHWA.

Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu (kushoto) akikanusha kukamatwa na rushwa na takukuru wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bunge mjini Dodoma  leo.Kulia ni Mbunge wa Mafia Abdurahman Shah.

Na.Mwandishi wetu Dodoma.

 Mbunge wa Ilala Musa Azan  Zungu leo amekanusha kukamatwa na Rushwa na takukuru kwenye mkutano mkuu wa jumuia ya wazazi  uliofanyika juzi. Zungu amesema kuwa magazeti yamekaririwa kupotosha ukweli kuwa yeye Zungu alikuwa amekamatwa na Rushwa.

Amefafanua kuwa yeye alisimamishwa na maafisa wa Takukuru na kupekuliwa  gari lake na kuchukua simu zake kwa ajili ya uchunguzi zaidi na siyo kukamatwa na maafisa hao Zungu ametaka magazeti hayo kuandika katika kurasa za kwanza habari za kukanushwa kwa kukamatwa kwake kinyume cha hapo atachukua mkondo wa sheria  mahakamani.

 Amedai  kuwa habari hizo zimesumbua jamii ya Tanzania, ndugu zake na wapiga kura wake wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam ukizingatia kuwa yeye ni kiongozi wa umma. Amesema kuwa habari hizi zimetumika kisiasa sana kwa nia ya kumchafua yeye asipite ujumbe wa NEC ya CCM kupitia jumuia ya wazazi.
CHANZO: Dewji Blog

0 comments:

Post a Comment