Mbunge Maalum, Sheikh Mohamed Dor, amekamatwa na maafisa wa upelelezi , CID, kutokana na uhusiano wake na vuguvugu la MRC, hususan ufadhili wake. Dor amekamatwa leo asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Runda, hapa Nairobi, alipo zuiliwa na kuhojiwa .
Viongozi wa Kiislamu mjini Mombasa na hapa Nairobi hata hivyo wamejitokeza kukashifu kukamatwa kwa Dor wakidai matamshi yake kuhusiana na vuguvugu la MRC sio kinyume cha sheria, huku wakipanga kikao hapo kesho kujadili mwelekeo watakaochukuwa endapo hatawawekwa huru.
SOURCE: CLICK




0 comments:
Post a Comment