SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, September 25, 2012

Wanafunzi wa Ilboru waandamana, Naibu Waziri azuru na kumsimamisha kazi Mwalimu mlevi

Naibu waziri wa elimu na ufundi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI akiwa anaongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilboru



Leo, Jumanne, Septemba 25, 2012 - 
Woinde Shizza, Arusha
 ==== 
Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mwalimu wa shule ya Sekondari ya vipaji Maalumu ya Ilboru Mkoani Arusha mara baada ya kukutwa akiwa amelewa shuleni hapo wakati wa kazi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kawaida shuleni hapo kutafuta ufumbuzi wa tatizo la wanafunzi lililosababisha kuandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kugoma kuingia darasani.

Majaliwa alilazimika kufanya hivyo wakati akiongea na walimu wa shule hiyo juu ya chanzo cha mgogoro huo, ambapo mwalimu huyo, Potin Jovita Sumawe, alinyanyuka na kuanza kuongea kama mtu aliyechanganyikiwa mbele ya Waziri huyo,
“Nimemuagiza afisa utumishi kumpeleka hospitalini kwa ajili ya kupimwa kama anamechanganyikiwa na ripoti iliyoletwa kwangu ni kuwa alikuwa amelewa hivyo tunamsimamisha kazi na kuanza kupitia faili lake tuone kama anaweza kuonyeka ama la!”alisema Majaliwa.

Aliongeza kuwa watumishi wote hawatakiwi kwenda kazini wakiwa wamekunywa au wametumia kilevi cha aina yoyote huku akisisitiza kuwa mahali pa kazi sio mahali pa kunywa pombe na kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya utumishi wa umma, “Kama mtumishi wa umma anavunja sheria kwa kunywa pombe kazini atachukuliwa sheria kwa kuwa hata yule mtoto aliyekabidhiwa kumfundisha anamfundisha kwa misingi ipi? Wafanye kazi kwa maadili mema!” Alisema Majaliwa.

Aliongeza kuwa hii sio hapa tu bali sehemu yeyote mfanyakazi wa Serikalini au sekta binafsi haruhusiwi kufanya kazi akiwa  amelewa, hivyo mtu yeyote akikutwa katika hali hiyo, anastaili kufukuzwa kazi.

0 comments:

Post a Comment