Mtafiti mchambuzi uwazi Twaweza Tanzania Bw.Nyankomo Marwa akiongea na waandishi wa habari jana (hawapo pichani) katika ofisi ya taasisi hiyo jijini Dar es salaam kuhusu kutoridhika na Hospital zinazotoa huduma kwa wagonjwa pindi wanapo kwenda kupata huduma za matibabu (kulia kwake)Afisa mawasiliano na utetezi Tanzania Bw.Risha Chande
.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE).
Na Datus Boniface.
Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza, limeweka wazi utafiti waliyoufanya wenye lengo la kuelewa namna ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanavyofikiria kuhusu huduma na utendaji wa Afya na kusema, Wananchi wamekuwa wakitoa rushwa ili kupata huduma hiyo kwenye hospitali za serikali.
Mtafiti Mchambuzi wa Twaweza Nyankomo Marwa, amewambia waandishi wa habari jijini kuwa, rushwa imetumika kwa kiasi cha asilimia 19 katika vituo vya afya vya serikali katika mwaka uliyopita.
Amesema licha ya kutoa rushwa kwa ajili ya kupata huduma za afya, pia serikali imeweza kutekeleza sera mbalimbali za afya ikiwemo matumizi ya vyandarau kwa Wananchi wake, kwani utafiti unaonyesha kwamba asilimia 95 ya wakazi wana chandarua.
CHANZO: BOFYA
0 comments:
Post a Comment