SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, September 1, 2012

Meneja wa 50 Cent Na Mariah Carey, Chris Lighty Ajiua


Meneja wa muda mrefu wa 50 Cent, Diddy, Ja Rule, na Mariah Carey, Chris Lighty amepatikana akiwa amekufa jana asubuhi jijini New York katika kile kinachoonekana kama kajiua kwa kujipiga risasi.
Kwa mujibu wa polisi, mwili wa meneja huyo aliyekuwa na miaka 44 ulipatikana saa 11:30 AM kwa saa za Marekani kwenye nyumba yake ya Bronx. Kifo hicho kinachunguzwa kama kitemetokana na kujiua mwenyewe.
Kwa mujibu wa vyanzo, Lighty, alikuwa na majibizano na mke wake wa zamani na kuamua kujipiga risasi kichwani.
Yeye na mke wake walipeana taraka mwaka jana.
Mastaa wengi wameonesha kushtushwa kutojana na kifo hicho huku Rihanna akiandika, “Rest peacefully Chris Lighty, my prayers go out to family and loved ones! Dear God please have mercy.”

0 comments:

Post a Comment