SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, September 15, 2012

KIKAO CHA NANE CHA TATHMINI YA SENSA CHARIDHISHWA NA ZOEZI HILO LILIVYOFANYIKA.

Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Balozi Seif Ali Iddi akiendesha kikao hicho kilichokutana Zanzibar. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha , Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee na kushoto ni Waziri wa Fedha wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Dkt. William Mgimwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akichangia mada katika Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichofanyika Zanzibar.
Baadhi na Mawaziri wa SMT ambao ni wajumbe  wakiendelea na Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi hapo Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Kikao cha Nane cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania kimekutana chini ya Mwenyekiti wake Mweza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu na Baadhi ya Maafisa wa Takwimu bara na Zanzibar walipata fursa ya kutathmini mwenendo mzima za zoezi la kuhesabu Watu Nchini Lililomalizika mwishoni mwa Wiki iliyopita.
Akitoa Tathmini ya zoezi hilo la Sensa kwa Upande wa Tanzania Bara Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. William Mgimwa amesema kwa sasa kazi ya kuhakiki usahihi na kuhariri taarifa zilizokusanywa na Makarani wa Sensa zinaendelea Nchi nzima kwa kutumia miongozo iliyotolewa na Wizara husika.
Dkt. Mgimwa amesema wasimamizi katika ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya walikuwa na kazi ya kuhakikisha madodoso ya maeneo yote ya kuhesabia watu katika wilaya zote yameshakusanywa ili kukamilisha awamu ya pili ya Sensa ya watu na makazi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee akitoa thathmini kwa upande wa Zanzibar amesema juhudi zinaendelea za kuimarisha ubora wa kupata idadi ya Watu na kuhakiki madodoso ili kuwa na Takwimu sahihi kwa maendeleo ya Taifa.
Mh. Omar Yussuf ameeleza kwamba  ipo haja ya kutafutiwa ufumbuzi mambo yatayoathiri ubora wa takwimu kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchambuzi wa Takwimu hizo.
Wakichangia wajumbe wa Kikao hicho  wamewapongeza Makarani, wasimamizi pamoja na watendaji wote waliosimamia kuendesha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana na Mwakilishi wa Jumuiya Aga Khan Foundation aliyepo Zanzibar Bw. Mohd Baloo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Jumuiya hiyo yenye Makao yake Makuu Mjini Geneva kwa dhamira yake ya kusaidia Maendeleo ya Zanzibar hasa katika harakati za uimarishaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Balozi Seif amesema mchango wa Jumuiya ya Aga Khan ndani ya  Mji Mkongwe wa Zanzibar umepelekea ushawishi wa kuwa na mvuto kwa wageni pamoja na watalii wanaotembelea Zanzibar na hatimae kuongeza mapato ya Taifa pamoja na ajira kwa baadhi ya Vijana kupitia Sekta ya Utalii.
Mapema Mwakilishi wa Jumuiya ya Aga Khan Foundation Zanzibar Bw. Mohd Baloo alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Taasisi yake imekuwa ikijihusisha mara kwa mara na ustawi wa Jamii katika Mataifa mbali mbali Duniani.
Bw. Baloo amesema Jumuiya hiyo bado inaendelea na mipango ya kuongeza miradi yake ya Kiuchumi itakayosaidia ustawi wa Kiuchumi katika Mataifa washirika Duniani.
CREDIT TO dewjiblog

0 comments:

Post a Comment