Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilali akihutubia Mkutano wa Kumi na Sita wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na Siasa ya Upande wowote unaomalizika leo mjini Teheran, Iran. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine alisisitiza msimamo wa Tanzania kuendelea kupigania haki, kutetea wanyonge, kupinga ubeberu na ukandamizaji kote duniani, pia aliiasa Jumuiya ya Kimataifa kutatua migogoro yote kwa njia ya amani.
Maafisa mbalimbali wa serikali walioongozana na Makamu wa Rais nchini Iran wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment