SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 13, 2012

BALOZI SEIF ALI ATOA MCHANGO WAKE KATIKA UJENZI WA SHULE KIJIJI CHA MBUYUNI KISIWANI PEMBA.

 
 Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ya mradi wa skuli ya  Istiqama uliopo katika kijiji cha Mbuyuni Mkoani Pemba Ustadhi Mohd Omar Makame akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea mradi huo. Kushoto ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.      
    
Mjumbe wa Kamai Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa shilingi 800,000/- kusaidia ununuzi wa saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Tawi la CCM la Makombeni Mkoani Kisiwani Pemba. Sambamba na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pia akakabidhi mchango wa shilingi 300,000/- kwa ajili yha milango ya Tawi hilo.
Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi la CCM, Makombeni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif Ali Iddi aliyetembelea Tawi hilo kuangalia hatua iliyofikia ya ujenzi wa Tawi hilo.

====
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono miradi yote inayoanzishwa na Taasisi, Mashirika, Jumuiya na hata Wananchi kwa lengo la kustawisha Maendeleo ya Jamii Nchini.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati akikagua mradi mkubwa wa ujenzi wa shule inayojengwa na kusimamiwa na Jumuiya ya Istiqama Tanzania katika Kijiji cha mbuyuni Mkoani Kisiwani Pemba.

Balozi Seif ameuambia uongozi wa wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa mradi huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kwamba miundo mbinu muhimu ya maji, umeme na bara bara inawekwa ili kufikia lengo lililokusudiwa la kuanzishwa kwa mradi huo muhimu kwa jamii

Ameuagiza Uongozi huo kumuandikia barua mara moja ya changamoto wanazopambana nazo ambazo zimo ndani ya uwezo wa Serikali Kuu ili iwe rahisi kwake kuziagiza Taasisi husika kupanga mikakati ya kutekeleza miundo mbinu hiyo.

Balozi Seif amesema atatumia uwezo na nafasi aliyonayo kushawishi wahisani zikiwemo ofisi za Kibalozi kusaidia ujenzi huo uliolenga kwenda hadi ghorofa tatu ambao tayari hivi sasa umeshatumia karibu shilingiMilioni mia tatu ( 300,000,000/-).

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Jumuiya hiyo ya Istiqama Tanzania kwa hatua yake ya kujenga mradi huo mkubwa ambao utasaidia kusukuma mbele Maendeleo ya Elimu ya Dini na Dunia.

Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Mradi huo Ustaadhi Mohammed Omar Makame alimueleza Balozi changamoto wanazopambana nazo wakati huu wa ujenzi.

Ustaadh Mohd Omar alizitaja changamoto hizo kubwa kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya maji safi, umeme pamoja na Barabara licha ya juhudi walizochukuwa za kuchimba kisima bila ya mafanikio.

Alisema ujenzi wa shule hiyo ulioanza tarehe 1/12/2010 utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 1575, Madarasa 45 , mabweni, nyumba za walimu pamoja na msikiti lengo likiwa kunyanyua elimu ya dini sambamba na kuibua vipaji vya wanafunzi.

Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi huo pamoja na uhai wa Chama Katibu wa CCM wa Tawi la Makombeni Bibi Wahida Mbaraka Mohd alisema ujenzi wa Tawi hilo umekuja ili kwenda sambamba na hadhi ya chama chenyewe kilivyo.

Bibi Wahida alisema hadi sasa ujenzi huo uliolenga kufikia gharama ya shilingi milioni 13,920,000/- umeshafikia shilingi milioni 8,000,000/-.

0 comments:

Post a Comment