Hospitali katika eneo la kaskazini magharibi mwa Iran ambalo limetokea tetemeko la ardhi, zimefurika wagonjwa waliojeruhiwa na tetemeko hilo, ambapo maaafisa wa nchi hiyo wameongeza juhudi za uokoaji katika eneo karibu na Tabriz.
Wizara ya Afya nchini humo imesema tetemeko hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita limeuwa watu zaidi ya 220 na kujeruhi wengine zaidi ya 300.
Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 6.4 kwenye kipimo cha Richter.
Maelfu ya watu wameachwa bila umeme wala makazi huku matetemeko madogo yakiendelea kutokea katika eneo hilo.

0 comments:
Post a Comment