MKATIBU mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis Suleiman Dadi (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo Majura ambaye pia ni mdau mkubwa wa michezo nchini.
Bulembo akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kuchukua fomu leo.
MDAU wa michezo nchini Abdallah Majura Bulembo amejitosa kuwania uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Bulembo ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA) na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alichukua fomu hizo na kuzirejesha jana hiyohiyo.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hizo, Bulembo alisema kwamba amelazimika kuwania nafasi hiyo ili kuifanyia makubwa jumuiya hiyo kwani ni mwanachama halali wa CCM na mwenye sifa hivyo anawajibu wa kuwania nafasi yoyote inayomfaa kwa lengo la kuendeleza mikakati iliyopo ndani ya jumuiya hiyo.
Hata hivyo, Bulembo ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea nafasi hiyo na kushika nafasi ya pili nyuma ya Balozi Athuman Juma Mhina ambaye sasa ni marehemu, alisema ataweka wazi mikakati yake pindi atakapopitishwa na halmashauri kuu ya CCM.
Bulembo anakuwa mgombea wa saba kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ambapo awali wanachama waliojitosa ni pamoja na John Edward Machemba, Said Ramadhan Bwanamdogo, Salim Hamis Chikago, Jasson Samson Rweikiza, Alfred Joseph Mwambeleko na Alphonce John Siwale.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Hamis Suleiman Dadi,alisema zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu wa nafasi mbalimbali katika jumuiya hiyo lililoanza Agosti 22 litafikia tamati Agosti 29 mwaka huu.
Alisema mbali na nafasi ya uenyekiti, tayari baadhi wa wanachama wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongoizi katika jumuiya hiyo kwa upande wa Bara na Visiwani.
Alizitaja nafasi nyingine ni pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Bara na Zanzibar, Wajumbe wa Kamati Kuu Wazazi kwa upande wa Bana na Visiwani, Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja wa Vijana (CCM).
HABARI/PICHA NA dinaismail.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment