Mwenyekiti mpya wa Tawi la Chadema Washington DC, Ndugu Cosmas Wambura akiongea mambo machache baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya.
Aliyekuwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Kalley Pandukizi akimkabidhi Kitabu cha Katiba na Sera za Chama Mwenyekiti mpya Ndugu Cosmas Wambura.
Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington, Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.
Kutoka kushoto: Katibu mpya Isidory Lyamuya, Mwenyekiti mpya Cosmas Wambura, Katibu aliyemaliza muda wake Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi.
Baadhi ya wanachama wa Chadema walioshiriki zoezi la Uchaguzi la kupata Viongozi wapya wa Chadema Washington DC.
-----
Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokuwa Viongozi wa muda. Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi. Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine zilizogombewa ni Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee. Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbali za kukijenga Chama. Pia Katibu mpya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote kuhakikisha Chama kinazidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.
0 comments:
Post a Comment