Katibu mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard akionyesha kibali cha polisi kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo leo
Polisi Iringa Ruksa wanahabari kuandamana kesho.
katibu wa IPC Frank Leonard akizungumza na wanahabari katika ofisi za IPC leo juu ya maandamano yao kesho.
Mtangazaji wa Ebony Fm Raymond Francis (kulia) katibu wa IPC Frank Leonard ,mtangazaji wa Nuru FM Sagi ,mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na mweka hazina wa IPC Vicky Macha wakielekea ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa leo.
Mmiliki wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Chama Cha Waandishi Wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) kushoto akiwa ameongozana na mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi ,Mtangazaji wa Nuru FM Bw.Sagi na mtangazaji wa Ebony Fm George Ndamagoyo kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa leo baada ya kuomba kukutana bila kuafikiana .
****
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limebariki maandamano ya wanahabari mkoa wa Iringa yaliyopangwa kufanyika kesho majira ya saa 4 asubuhi katika mji wa Iringa.
Katika kibali hicho kilichotolewa na jeshi la polisi leo asubuhi kabla ya kutolewa lilikutana na katibu wa IPC Frank Leonard kuomba kufanya marekebisho ya njia na kukubaliana na kuifuta njia ya Uhindini na badala yake kuruhusu maandamano hayo kutumia barabara ya Uhuru kutoka Bustani ya Manispaa ya Iringa kwenda barabara ya samora na kuishia kanisa la RC mshindo na baada ya hapo kurudi kwa kupita barabara ya Mashine tatu ,Stendi kuu ,M.R Hoteli na kuishia ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa.
Katika barua hiyo ya jeshi la polisi yenye kumbukumbu namba IRI/A./14/VOl.x11/178 iliyotumwa kwa mtendaji mkuu wa Iringa Press Club yenye kichwa cha Maombi ya kibali cha kufanya maandamano ya amani
Imeanza kwa kusema tafadhali rejea barua yako kumb. IPC/02/o12/ Machi 2 ya 03/03/2012 inayohusu kichwa cha habari hapo juu.
Kibali kimetolewa cha kufanya maandamano ya amani kwa Klabu ya wanahabari mkoa wa Iringa mnamo tarehe 6/3/2012 muda wa saa 4 asubuhi kama ifuatavyo maandamano hayo yataanzia kwenye bustani ya manispaa ya Iringa kuelekea kanisa la Mshindo kwa kupitia barabara ya Uhuru.
Baada ya kufika kanisa la Mshindo watapita barabara ya Ubena Club kuelekea stendi kuu ,MR Hotel,Luxury hadi ofisi za mkuu wa mkoa ambapo yataishia .
Nakala kwa RPC Iringa kwa taarifa na RTO tafadhali panga askari wa kuongoza maandamano hayo
Nawatakia maandamano mema Mkuu wa polisi wilaya ya Iringa MOhamed Mkwazu Semunyu
Tayari mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ambaye alipaswa kupokea maandamano hayo amekutaka bila kufikia makubaliano na wawakilishi wa wanahabari mkoa wa Iringa katika kikao kilichoanza majira ya saa 6 mchana hadi saa 8 huku mkuu huyo wa mkoa akionyesha kuhofu maandamano hayo kwa madai kuwa ujumbe utakaoandikwa katika mabango unaweza kuchafua hali ya hewa .
Wakati huo huo Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC) kimepongeza hatua ya chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa(IPC) kutangaza maandamano ya kupinga manyanyaso yanayofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwa wao pia wapo pamoja na wanahabari hao kupinga hali hiyo.
Katika salamu zake za kupongeza uamuzi huo uliofikiwa na IPC mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Mbeya Bw Christopher Nyanyembe amempongeza mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na viongozi wote wa IPC kwa kuamua kusimama kidete kupinga vitendo vya wanahabari kuendelea kubaguliwa na kunyanyaswa na ofisi ya mkuu huyo wa mkoa na taasisi zake.
Kwani amesema kuwa kumekuwepo na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya mikoa hapa nchini kwa ofisi za wakuu wa mikoa kutenga wanahabari na kuwanyanyasa wakati wanapofanya kazi zao.
Alisema kuwa iwapo ofisi ya mkuu wa mkoa inatoa mialiko kwa wanahabari kwa ajili ya shughuli zake vikiwemo vikao vya kamati za ushauri za mkoa (RCC) na ziara za viongozi hao wilayani ni wajibu kwa mwanahabari kulipwa kwani hakuna chombo kinachotenga bajeti kwa ajili ya mwanahabari kushiriki viara ya kikazi ya mkuu wa mkoa ama kiongozi mwingine yeyote wakiwemo viongozi hao wa kitaifa.
Hivyo alisema kuandamana kwa wanahabari hao mkoa wa Iringa kutawafungua wanahabari wengine kote nchini kuungana na wanahabari mkoa wa Iringa katika kupinga vitendo vya ofisi za wakuu wa mikoa kuendelea kunyanyasa wanahabari.
WAKATI wanahabari mkoani Iringa kesho jumanne wamepanga kufanya maandamano ya amani majira ya saa 4 asubuhi kupinga ubaguzi na ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari kufanya kazi yake ,unyanyasaji unaofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa, chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimepanga kukutana na viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) asubuhi ya leo ili kusikiliza madai yao.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza ameomba kukutana na viongozi wa IPC ili kuweza kuyapata kiundani madai hayo na kuangalia kabla ya CCM kufika ofisi ya mkuu wa mkoa kuangalia uwezekano wa kumaliza tofauti hizo.
Kwani alisema CCM haiungi mkono suala la vyombo vya habari kutengwa ama kunyanyaswa wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi na kuwa CCM na jamii inategemea vyombo vya habari kupata taarifa mbali mbali.
Kiponza alisema kusudi la kukutana na viongozi hao wa wanahabari katika ofisi yao leo si kwa ajili ya kuzuia maandamano hayo bali ni kwa ajili ya kusikiliza madai yao na kuwa suala la wanahabari kudai haki yao ni wajibu wao ambao wao kama chama hawawezi kuingilia kati .
Mbali ya mwenyekiti huyo mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM pia ameeleza kusikitishwa na vyombo vya habari mkoani Iringa kuendelea kunyanyasika na kubaguliwa wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa na kuwa kwa upande wake hakupendezwa na manyanyaso waliyofanyiwa wanahabari hao wakati wa ziara ya makamu wa Rais na kuwa alimwagiza katika wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha kukutana na wanahabari hao .
Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya uongozi wa mkoa kuwalaza nje wanahabari hao wakati wa ziara ya Rais Kikwete wilaya ya Njombe na ziara ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghirib Bilala aliyefanya ziara yake katika wilaya ya Makete ,Njombe ,Mufindi na Iringa hivi karibuni.
Akitoa taarifa mbele ya wanahabari katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa leo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi alisema kuwa wanahabari wamekuwa ni watu wa kutetea makundi mbali mbali katika jamii ila wao wamekuwa nyuma kujitetea hata pale wanaponyanyasika .
Hivyo alisema wakati umefika kwa wanahabari kuanza kufunguka na kudai haki zao pale zinapoonekana kupokwa na watu wachache kwa masilahi yao .
Kwani alisema mkoa wa Iringa na vyombo vyake umekuwa ukiongoza kwa kuvibagua vyombo vya habari wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa na wakati mwingine kuwataka wanahabari hao kuchangia gharama za ziara hizo iwapo wanataka kushiriki ziara husika .
Mwangosi alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia afisa habari wake Denis Gondwe kutoa mialiko kwa wanahabari hasa pale mkoa unapohitaji kufikisha taarifa mbali mbali kwa wananchi ila inapotokea ziara za viongozi wa kitaifa ama mkuu wa mkoa kufanya ziara amekuwa akibagua vyombo vya habari na kutumia chombo cha serikali pekee
Alisema katika ziara ya Rais Kikwete waandishi waliopata kushiriki ziara hiyo walinusurika kulala kwenye gari kabla ya paroko kuwatafutia vyumba ila katika ziara ya juzi ya makamu wa Rais pia mkoa ulitoa usafiri huku ukitaka waandishi hao kuomba fedha za kugharamia ziara yao kutoka katika vyombo vyao hali iliyopelekea wanahabari hao kukosa maeneo ya kulala wala kula wakati wote wa ziara hiyo.
"Mkuu wa mkoa anapaswa kufanya kazi katika wilaya zote za mkoa wa Iringa kwa mshahara anaulipwa kila mwezi ......ila leo mkuu wa mkoa ama kiongozi mwingine wa wilaya anapofanya ziara katika eneo lake anajilipa posho ila mwanahabari anapoongozana na viongozi hao anaambiwa alipiwe na chombo chake kwa kazi ya ofisi ya mkoa"huu ni unyanyasaji mkubwa
Kwani ni kweli vyombo vy habari vinatoa fedha kwa wanahabari wao kwa ajili ya kwenda kuandika habari zile ambazo chombo cha habari inazihitaji kwa wakati huo mfano kama kuna ufisadi umefanyika katika Halmashauri husika ama kuna ajali /maafa yametokea ila sio kwa kwenda kushiriki ziara ya mkuu wa mkoa.
Alisema kuwa umefika wakati wa wanahabari mkoa wa Iringa kugoma kutumiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa badala ya kuwatumikia wananchi ambao ndio waajiri wakuu wa wanahabari hao kwa kuandika kero za wananchi
Kuhusu maandamano hayo alisema kuwa yamepagwa kuanzia viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa na kupita mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kwa kuelekea uwanja wa Samora kabla ya kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa .
Hata hivyo Mwangosi alisema wanahabari hao wataandamana wakiwa wamefunga midomo yao kwa plasta huku gari ya muziki likifuata kwa nyuma likiwa na wimbo maalum wa kudai uhuru maarufu kama ' Freedom is Coming Tomorrow'
Alisema kuwa wanahabari mkoa wa Iringa wamechoshwa kunyanyaswa na ofisi ya mkuu wa mkoa na mara nyingi ofisi hiyo ya mkuu wa mkoa wa Iringa imekuwa ikidai kuwa serikali haina pesa jambo ambalo kimsingi ni sawa na kuishusha heshima serikali ya Tanzania .
Mwangosi alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa imekuwa ikidai haina fedha za kulipia malazi na chakula kwa wanahabari huku msafara mfano wa makamu wa Rais ukiwa na magari zaidi ya 35 na viongozi wote katika magari hayo hadi madereva walilipwa posho ila wanahabari na askari polisi waliambiwa serikali haina pesa za kuwalipa
Aidha alisema kuwa katika maandamano hayo wanahabari watatoa tamko lao pamoja na mapendekezi kwa ofisi ya mkuu wa mkoa kama itaona kuna haja ya kudumisha mahusiano yake na wanahabari ama kupuuza .
Na Francis Godwin Mzee Wa Matukio

0 comments:
Post a Comment